KIFO CHA NGWEA.M TO THE P ANAENDELEA VIZURI

HABARI NA MILLAD AYO,JOHHANESSBUG

Mpaka sasa bado unaendelea utaratibu wa kusafirisha mwili wa Marehemu Albert Mangwea kutoka Johannesburg, South Africa, kutoka kwenye mochwari ya serikali ya Hillbrow.

Mangwea alifariki dunia 28 May akiwa Johannesburg, alipokuja kufanya show ambazo Watanzania wa huku wanasema mara ya mwisho kuonekana kwenye stage ilikua wiki tatu zilizopita.

Bado chanzo cha kifo hakijajulikana na bado pia majibu ya uchunguzi wa Madaktari hayajatoka ila tayari baadhi ya Watanzania walipata nafasi ya kwenda kutazama mwili wake kwenye mochwari ya Hillbrow ambapo ameonekana ametokwa na damu nyingi sana puani.


Gharama za kusafirisha mwili wake kutoka South Africa ni zaidi ya $3500 ambazo bado haijawa rahisi kupatikana kwake, lakini juhudi zinafanyika ili kufanikisha.

Kumekua na habari mbili kubwa zinazoenea kwamba msanii rafiki aliepelekwa hospitali pamoja na Ngwea, yaani M2theP, amefariki na pia ripoti ya madaktari imetoka.

Zote hizo ni habari za uongo, ripoti ya daktari bado haijatoka na pia M2theP hajafariki dunia, ni mzima wa afya na amekua akiendelea vizuri.

Ameanza kufungua macho toka jana na hata kunyanyua miguu, kitu ambacho manesi wamesema ni matumaini kama akiendelea hivyo ndani ya siku tatu anaweza kuanza kuongea.


Watanzia wakiwa na kikao cha kusafirisha mwili wa marehemu
Share:

BREAKING NEWS MATOKEO YA KIDATO CHA 6 YATANGAZWA

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YANATANGAZWA!
Baraza la mitihani hivi sasa linatangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2013. Matokeo hayo yatapatikana muda mfupi ujao kwenye tovuti yetu.
Asilimia 93 ya waliofanya mtihani huo wa kidato cha 6 wamefaulu.
Shule ya kwanza iliyoongoza ni Marian Girls ya mkoani Pwani na ya pili ni Mzumbe ya Morogoro.
Mwanafunzi wa 1 wa kiume kwa sayansi ni Erasmi Inyase kutoka Ilboru, na kwa wasichana ni Lucylight wa Marian girls.
Upande wa masomo ya Biashara mwanafunzi wa 1 ametoka shule ya Tusiime anaitwa Erick Robert.
Wanafunzi 89 matokeo yao yamezuiliwa kwa sababu mbalimbali.
Wanafunzi watakaothibitika kuwa walikuwa na matatizo ya kiafya, watapewa nafasi ya kurudia mtihani
Matokeo hayo yatapatika katika link muda mfupi ujao 
Share:

JINSI YA KUCHANGIA PESA KWAAJILI YA MAZISHI ALBERT MANGWEA

Jinsi ya kuchangia Pesa kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Albert Mangwea:Kwa yeyote uliyeguswa na msiba wa msanii,ndugu yetu Albert Mangwea unaweza kuchangia pesa kufanikisha mazishi kwa kutuma chochote ulichonacho kupitia hii
 ACC:NMB 2012505840 ambayo ni ya kaka yake anayeitwa Mangwea Keneth. 
Tigo Pesa 0717 553 905.
M PESA 0754 967 738 zote ni za kaka wa marehemu

.Msiba uko Mbezi Beach Goig DaR
Share:

SABABU ZA P FUNK KUKATAZA NYIMBO ZA NGWEA ZISIPIGWE CLOUDS

Kutoka na exclusive interview kati ya P FUNK na DAN CHIBO wa TBC,P FUNK alifunguka na kusema sababu za kukataza nyimbo za Ngwea zisipigwe clouds fm
Ilikuwa hivi

Leo nilipata fursa ya kuongea na mmoja kati ya maproducer wakongwe kwenye tasnia ya Muziki wa hapa Bongo aitwaye P Funk Majani. 
Mahojiano yalikuja mara baada ya taarifa zilizosambazwa mapema leo kwamba Producer huyo amekataza nyimbo zilizorekodiwa na Mwanamuziki aliyefariki nchini Afrika Kusini jana Albert Mangwea kuwa zisipigwe kwenye kituo cha Clouds Fm.

Mbali na mambo mengine nilitaka kujua ukweli na undani juu ya taarifa hiyo na haya ndio yalikuwa maongezi yangu na P Funk Majani...



DC: Je ni kweli kwamba umekataza Nyimbo za Ngwear zilizorekodiwa Bongo Record kuwa zisipigwe Clouds Fm..?

P Funk Majani: Hiyo ni kweli kabisa, mimi nimekereka na hili jambo kwanza kwa sababu mimi na Mangwea tumejuana miaka kibao na tumeongea mengi, so mimi nnachojua uamuzi niliochukua ni kitu ambacho yeye mwenyewe angependa na angetaka iwe hivyo....


Kwa sababu kila siku alipokuwa anakuja studio malalamiko yake ilikuwa ni kuhusu hawa hawa watu kila siku....

Umenielewa..? so ni hicho kilichokuwa kinatajika kufanyika, na mi mwenyewe sifurahi wao wafaidike, sasa hivi ambaye amefariki mtu wetu ambaye tunampenda nyie mnachukulia biashara wanatangaza, wanafanya nini, wanapiga na nyimbo, alipokuwa hai mbona mlikuwa hamumsaidii....



Mlipokuwa mnajua labda ana matatizo ya kutumia madawa ya kulevya mbona hamjamsaidia kumsaidia kumchangia kama Ray C sijui nani kumpeleka nje au wapi asafishwe basi......

So…! Vitu kama mimi basically nimechoka utawala wao sababua wao mchezo wao ni kuchezea wasanii vichwa kuwapa stress na kuwaangamiza kimaisha.....

Umenielewa… kwa udulumati wao, udhulumati wao umezidi so ndio hicho kinachosababisha watu wahanganyikie kimaisha, umenielewa…?


Kukosa fedha na kuweza kutimiza mahitaji ya maisha lazima uchanganyikiwe, unakimbilia vitu vitu suala za pombe au sijui madawa ya kulevya au nini inategemea na mtu moyo wako una nguvu kiasi gani cha kudhibiti hivi vitu.



DC: Unataka kusema kwamba jamaa ndio wamesababisha kifo chake…?


P Funk Majani: Siwezi kusema asilimia 100 wamesababisha lakini mchango mkubwa wa frustration, frustration, unajua kitu frustration…? Siwezi ku-accuse, si-accuse lakini hiyo ni maoni yangu mimi, kutokana na yale maongezi niliyokuwa nae nikikaa na mdogo wangu Mangwea, umenielewa….?

Najua kabisa alichokuwa ananiambia na vitu ndio vimemsababisha aingie huko, sasa mimi ndio sitaki kwa ufupi, kama nimekosea mtanisamehe bwana….

DC: Je umewataarifu rasmi..?

Nimeanza kwa kupiga simu kwa sababu ni asubuhi nimeamka vile nimewafahamisha, nimewaambia vizuri, nilivyowaletea hizi nyimbo niliwaletea bila mkataba au karatasi yoyote mmezipiga....


So... kwa sasa hivi kwa ustaarabu naomba nnavyowaomba acheni msizipige, na mi ntaleta official barua, nimeshaongea na Cosota, eeh watai-stamp Wakili ndio ataiandika barua inapelekwa vizuri na vitu vinaendelea, kama wao ni wastaarabu itabidi waelewe.
Share:

BREAKING NEWS-M TO THE P AMEAMISHWA KUTOKA WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI

HABARI KUTOKA JOHANNESBUG NA MILLAD AYO

"M TO THE P meshatoka katika wodi ya wagonjwa mahututi hapa johannesbug na ameshaanza kupata kumbukumbu.Ambapo alipouliza ngwea yupo wapi alijibiwa ngwea katangulia nyumbani TANZANIA.

M to the P bado hajaanza kula chakula zaidi anakunjwa vimiminika kama vile juice.

Mmoja wa watu wa karibu na ngwea ,SA GOD alisema kuwa "nimeishi na Ngwea kwa zaidi ya wiki mbili hapa Johhanessbug na Ngwea alihairisha mara 3 kurudi Tanzania.
Share:

MESEJI ZA MWISHO ZA NGWEA KWA WEMA SEPETU

Ngwea alikuwa anapanga Kumtumia mwadadada mwingine wa bongo movies Kajala Masanja kwenye video yake mpya aliyokuwa anajiandaa kuifanya. Maongezi yao yalikuwa hivi.
Mangwea : kuku bandani..
Mangwea : Nataka Kajala…
Mangwea : Sikiza nyimbo then utanipa idea..
Mangwea : Nataka tukipiga hela kwa bro…
Mangwea : Tulipe na hela ya ticket ya Jux aje toka China tumalize huku kusini
Mangwea : #hugs
Wema Sepetu : Upo api?
Mangwea: Me nipo Pretoria now momo…

Share:

Breaking news-M to the P ANAENDELEA VIZURI

Kutokana na taarifa zilizotapakaa katika vyombo vya mbalimbali ni kuwa m to the p amefariki pia lakini maelezo ya daktari akiongea na clouds fm leo amethibitisha kuwa M to the P  anaendelea vizuri ingawa bado hajapata nguvu vizuri za kuongea.
Pia Millad Ayo aliongea moja kwa moja kutoka South Afrika alithibisha kumuona M to the P anaendelea vizuri

Kwa upande mwingine daktari amesema kuwa uthibitisho kuhusu kifo cha Ngwea bado haujajulikana bado wapo katika uchunguzi zaidi majibu yatatolewa baada ya uchunguzi kufanikiwa.
PICHANI NI NGWEA NA M TO THE P

MUNGU AMPE AFYA M TO THE P
R.I.P MANGWEA
Share:

MSIBA WA MANGWAIR "SHOW YA MWANA F.A YAHAIRISHWA"

Shows mbili zilizokuwa zifanyike ijumaa hii Tar 31 Mwezi wa tano zimehairshwa kutokana na msiba wa msanii maarufu ngwea,aliyefariki akiwa nchini South Africa mapema Mchana wa leo,Mwana FA akiongea na kipindi cha ampilifaya cha clouds fm amesema kwamba wameamua kuhairisha show yao hiyo ikiwa ni heshima kwa msanii huyo,na akaongeza show itafanyika mara baada ya mazishi yake na tarehe mpya ya show hiyo itatangazwa  siku chache zijazo,Msanii kalapina wa kikosi cha mizinga naye ameamua kuhairisha show yao iliyokuwa ifanyike ijumaa hii pia

Share:

MAELEZO KUHUSU KIFO CHA MANGWAIR

KIFO CHA ALBERT MANGWAIR 28/May/2013, R.I.P!!!

HABARI KUTOKA KWA SAICO DOS

HABARI ZINASEMA KUWA alikuwa yeye na wenzake 3 yani walikuwa wa 4, Leo asubuhi walikuwa wanarudi Brixton wakitokea town Johanessburg,Ngwair tiketi yake ya ndege ilikuwa tayari kwa ajili ya safari Leo hii hivyo tulikuwa tayari kumsindikiza Airport Leo Asubuhi, hvyo wakamgongea mlango mshikaji akawafungulia, waliingia ndani lakini walikuwa wamelewa, sasa ikawa wanaendelea kula mambo yao ndani,ghafla Mangwair akaanza kujisikia vibaya, then akaanguka chini na kupoteza faham wakaona kama anafanya masihala, hali hiyo iliendelea hadi mida ya saa sita mchana ikawa mbaya zaidi pia jamaa mwingine nae akapoteza fahamu hvyo hvyo coz walizidisha mambo kutumia,tukaitwa kumchek ikabd tuogope mpaka mida ya saa nane mchana ilibd tumpigie simu jamaa fulan Msouth Africa ni Taxi Driver ili tumpeleke Hospital coz sis tuliogopa kumpeleka na magar yetu Binafsi, akaja tulimchukua pamoja na yule mwingne had hospital kufika kule Doctor kumchek alikuwa tayar ameshakufa na yule mwingne bado yu hai ila hali yake sio nzur, ilibd jamaa Kat yetu aka sign kuhusiana na kufa kwa Albert Mangwair hvyo kesho Doctor atatupatia karatas ili tukabdhiwa mwili wake kwa ajr yakuusafirisha Tanzania!! Hivyo Ndvyo ilivyokuwa had kufa kwa Albert Mangwair mwili wake upo Helen Joseph Hospital in Hursthill next to Aukland park and University of Johannesburg, also Brixton and Westdene in Johannesburg South Africa!!
Share:

BREAKING NEWS-DUDE AFIWA NA MAMA YAKE LEO ASUBUHI

HABARI KUTOKA BONGO MOVIE
Mwigizaji Kulwa Kikumba maafuru kama (Dude), msanii wa bongo movies,amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na mama yake mzazi asubuhi ya leo jijini Dar es salaam taarifa zimetufikia.
 Katika ujumbe wake ambao ameutuma kwa wadau wake, msanii huyo ameandika
“Ndugu zangu wapendwa, nimefiwa na mamaangu mzazi niliyempenda kuliko mtu yeyote kwenye dunia hii, leo . Inna Lillah waa inna illah rajiun”
Taratibu za mazishi zinafanywa na familia ya Marehemu na tutaendelea kwajulisha hapa hapa utaratibu wa mazishi.
Mungu ampe nguvu ya kuweza kusimama imara katika wakati huu mgumu kwake na familia yake kwa ujumla
(Pichani ni msanii huyo akiwa kwenye gari akimpeleka mama yake hospitalini kwa matibabu, kumbe mama huyu tayari alishakuwa ameiaga dunia)
Pole sana kaka Dude!

Share:

BREAKING NEWS _ALBERT MANGWAIR A K A COWBAMA AFARIKI DUNIA AFRIKA KUSINI

Taarifa nilizopokea hivi punde zinasema kuwa msanii maarufu wa hip hop Tanzania amefariki dunia akiwa nchini Africa kusini
Taarifa zaidi zitawajia baadae kidogo
Amefariki Leo Asubuhi.
Alikuwa Ghetto Moja Na Msanii M To The P.
Walivyokwenda Kuwagongea
Asubuhi Walikuta Ngwear
Amefariki Na M To The P
Amepoteza Fahamu Kabisa. Pia
Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa Watu Wa Karibu Wa
Ngwear Huko South Africa.
Wanasema Alilala Amelewa
Share:

DR.CHENI ALISHWA SUMU UKUMBINI

HABARI KUTOKA BONGO MOVIE

Katika hali ya kushangaza na isiyo eleweka mwigizaji Mahsein Awadhi maarufu kama Dr. Cheni amekumbwa na balaa la kulishwa chakula chenye sumu weekend iliyopita alipokuwa kwenye sherehe moja ya harusi jijini Dar es Salaam alipohudhuria kama MC au mshereheshaji wa harusi hiyo.
Akiongea na bongo movies leo asubuhi, Dr. cheni alisema kuwa baada ya kumaliza kula chakula ambacho alipakuliwa na mmoja wa wahudumu wa sherehe hiyo alianza kujisikia vibaya na kuishiwa nguvu na aliamua kutoka nje kujaribu kupata hewa akidhani ladba ni joto la ukumbini ila hali ilizidi kuwa mbaya na aliamua kutafuta maziwa akihisi labda inaweza kuwa vidonda vya tumbo ndipo alipoanza kutapika na baadae kukumbizwa hospitalini na ndipo alipogungulika kuwa amelishwa chakula chenye sumu.
Tulipomuuliza labda sababu gani anahisi zinaweza kuwa zimepelekea watu hao kutaka kumdhuru alisema kuwa, mpaka sasa hajaweza kupata jibu kamili ila anaamini watu waliofanya hivyo wanamfahamu na wana nia mbaya sana kwake na sio watu wema.
Dr. Cheni alisema kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na moja ya watu walikuwa wa kwanza kufika hospitalini baada ya yeye kupatwa na majanga hayo ni mwigizaji Elizabeth Michael (LULU) ambaye kwa sasa yupo karibu sana na Dr. Cheni aliyekuwa mstari wa mbele katika kushughulikia mpaka kufanikisha suala la dhamana ya kesi iliyokuwa inamkabili mwanadada huyo.
Share:

RUVUMA-WATU 8 WAMEFARIKI DUNIA KWA AJALI

Watu nane wamefariki dunia  baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo kwenda Songea  kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma .
Roli hilo lilikuwa limebeba magunia ya ufuta, mpunga wakiwemo na abiria

 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma  Deusdedit  Nsimeki amesema ajali hiyo imetokea jana Tarehe 26.05.2013 majira ya saa nne na nusu( 4:30 usiku  katika kijiji cha Hanga eneo la bombambili mkoa wa Ruvuma, chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi na dereva kuendesha gari akiwa amelewa,

Ajali hiyo  imehusisha gari lenye namba za usajili T.677 ADL  aina ya Isuzu lori , mali ya mfanyabiashara wa mazao maarufu kwa jina la Mtazamo. likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN NYONI mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI SONGEA,
Baada ya ajali hiyo kutokea dereva wa gari hilo amekimbia na kutelekeza gari porini hadi sasa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya jitihada za kumtafuta ili sheria ifuate mkondo wake.

Kamanda wa Polisi amesema gari  hilo liliacha njia baada ya kugonga daraja na kupinduka na kusababisha vifo vya watu nane(8)  na majeruhi kumi na moja (11) ambao
wote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.


Kutokana  na ajali hiyo mbaya kamanda wa polisi wa  Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya mizigo kutopakia mazao pamoja na abiria na atakayekiuka atachukiliwa hatua kali za kisheria.
Pia ametoa wito kwa wamiliki/wasimamizi wa magari kuwa wanatakiwa kuhakikisha magari ya mizigo,mazao hayapakii abiria na atakaye kiuka agizo hili hatafikishwa mahakamani mala moja 
ambapo

Share:

HIZI NDIO PICHA ZA WASHIRIKI 28 WA BBA"THE CHASE"


HAWA NI KUTOKA TANZANIA-FEZZA na NANDO

HAWA NI KUTOKA ANGOLA-BRAULIO na NEYLL

HAWA NI KUTOKA BOTSWANA-MOTAMMA na ONEAL

KUTOKA ETHIOPIA -BETTY na BIMP

KUTOKA GHANA -ELIKEM na SELLY


KUTOKA KENYA-ANNABEL na HUDDAH

KUTOKA MALAWI-FATIMA na NATASHA

KUTOKA NAMIBIA -DILISH na MARIA

KUTOKA NIGERIA -BEVERLY na MELVIN

KUTOKA SIERRA LEONE -MICHAEL na BOLT

KUTOKA SOUTH AFRICA - ANGELO na KOKETSO
KUTOKA UGANDA -DENZEL na LK4

KUTOKA ZAMBIA -CLEO na SULU

KUTOKA ZIMBABWE -HAKEEM na POKELLO
Share:

MATOKEO KIDATO CHA NNE 'UFAULU WAONGEZEKA'

Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
Share: