Posts

Showing posts from June, 2013

Video-Kili Music Tour: PROFESA JAY NA KALA JEREMIAH WAKIFREESTYLE

U.S EMBASSY TANZANIA "MAONI YA WATU KUHUSU KUJA KWA OBAMA"

CLICK LINK HAPA CHINI KUONA MAONI YA WATU KUHUSU KUJA KWA OBAMA

U.S EMBASSY TANZANIA-MAONI YA WATU

Makala Maalum-UJIO WA OBAMA TANZANIA NI KUFURU

Image
Ulinzi mkali ambao tayari upo na utazidi kuonekana wakati wa Ujio wa Rais wa Marekani umewafanya baadhi ya Watanzania kujihisi wanadunishwa au kuabishwa. Wapo wengine ambao wanaona kuwa hatua mbalimbali za kiusalama zinazochukuliwa kumlinda Obama, Familia yake na ujumbe wake zinaonesha dharau na kutoaminiwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi. Wengine wanafika mahali pa kuhisi kuwa Wamarekani wanatudharau sana kiasi kwamba wanatuchagulia nani aonene na Obama (rejea taarifa kwenye gazeti la Mwananchi la leo). Watanzania hawapaswi kujisikia hivyo hata kidogo.

Ulinzi wa Obama ni Mkali iwe ndani ya Marekani au Nje

Wakati wowote Rais wa Marekani anaposafiri iwe ndani ya Marekani au nje ya Marekani ulinzi wake ni mkali na karibu kamili (almost absolute). Kuanzia angalia ambalo anakuwepo (linakuwa no fly zone) na kuwa anaenda na kila kitu kinachoweza kutumika wakati wowote wa dharura yoyote inayoweza kufikirika kutokea. Kuanzia majanga ya moto, maji, maandamano ya kisiasa au hata mapinduzi ya kijes…

OBAMA , ZUMA ANA KWA ANA

Image
Rais wa Marekani Barack Obama, amesema uvumilivu na ujasiri wa Nelson Mandela ni mfano mwema kwa dunia na upendo wa dhati wa rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini inaonyesha ni kwa namna gani alivyo na utu wa kibinadamu.
Bwana Obama ameongeza kuwa Mandela, alionyesha ukweli na ukakamavu ambao una maana kubwa katika utu wa kibinadamu ambao uliondoa tabaka la ubaguzi, udini na utaifa.
Rais huyo wa marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria baada ya mazungumzo na rais wa sasa wa Afrika kusini, Jacob Zuma.
Ziara hiyo ya bwana Obama ina lengo la kuongeza mauhusiano ya kibiashara lakini imetekwa na hisia za ugonjwa wa bwana Mandela ambaye amelazwa hospitalini kwa muda wiki tatu sasa kutokana na maradhi ya mapafu yanayosumbua mfumo wake wa kupumulia.
Katika kikao hicho wawili hao walizungumza na vyombo vya habari kuhusu ushirikiano wa mataifa yao kibiashara mbali na kutafuta suluhu ya kudumu katika mataifa yaliokumbwa na ghasia mashariki ya kati.
Ikulu ya White House imesema kuwa Oba…

VIONGOZI WACHUJWA KUMPOKEA OBAMA

Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Pia alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu saa 8:40 mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo, kwa maana wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa siku mbili.

“Wamesema kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia wageni watakaoingia na kutoka na wataamua nani aingie na kutoka,” alisema Malaki. Imebainika kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.

“Wenyewe wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo katika kundi…

MAOMBI ZAIDI KWA MANDELA NJE YA HOSPITALI ALIPOLAZWA

Image
Mamia ya watu wanaendelea kukusanyika nje ya hospitali alikolazwa Nelson Mandela mjini Pretoria Afrika Kusini. Inaarifiwa Mandela bado yuko hali mahututi.
Wamekuwa wakimuimbia nyimbo na kumuombea nje ya hospitali. Wengine wamekusanyika katika iliyokuwa makaazi ya Mandela mtaani Soweto.

Afrika Kusini
Watu wana wasiwasi kuhusu hali y mandela lakini pia wanataka kuonyesha wanavyojivunia kiongozi wao ambaye wanamuona kama baba wa taifa lao.
Mandela , rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini, anaugua maradhi ya Mapafu.
Mamia ya wananchi walikesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe alisema afya ya babake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi n…

OBAMA KUTEMBELEA KISIWA ALICHOFUNGWA MANDELA MIAKA 27

Image
Rais Obama atazuru kisiwa cha Robben Island alikofungiwa jela rais wa zamani Nelson Mandela kwa miaka 27.
Rais wa Marekani Barack Obama leo Ijumaa anaelekea Afrika Kusini ambapo miongoni mwa shughuli zake atazuru kisiwa cha Robben Island  alikofungwa jela rais wa zamani Nelson Mandela kwa miaka 27. Rais Obama anakwenda nchini humo wakati bw. Mandela akiwa katika hali mbaya ya afya. Rais huyo wa zamani anatibiwa katika hospitali moja ya Pretoria. Alihamis rais Obama alisema ziara yake katika eneo ambalo watumwa wa Afrika waliondoka barani humo kwenda Amerika kaskazini imempa hamasa mpya ya kulinda haki za binadamu. Bw. Obama alitembelea kisiwa cha Goree kwenye ufukwe wa Senegal Alhamis. Wanahistoria wanasema maelfu ya Waafrika wanaume kwa wanawake wakiwa wamefungwa minyororo walishikiliwa huko na kupitia kile kilichoitwa mlango wa kutorudi tena kupanda meli ya watumwa wakielekea bahari ya Atlantic. Rais Obama alisema ziara yake katika kisiwa hicho ilimpa hisia kali na nafasi ya kutathm…

MASHIRIKA,WANAFUNZI WAPINGA ZIARA YA OBAMA AFRIKA KUSINI

Image
Huku Rais Barack Obama wa Marekani akiwa amewasili nchini Senegal hii leo katika duru yake ya kwanza ya safari barani Afrika, safari yake hiyo inakabiliwa na upinzani mkubwa huko Afrika Kusini ambayo itakuwa nchi ya pili kuitembelea kabla ya kuelekea Tanzania.
Duru zinaarifu kuwa idadi kubwa ya mashirika ya wafanyakazi, wanafunzi wa vyuo vikuu, mawakili na watetezi wa haki za binaadamu wanapinga vikali safari ya Rais Obama nchini humo. Muungano wa Jumuiya za Wafanya Kazi Afrika Kusini COSATU umewataka wafanyakazi nchini humo kufanya maandamano ya kupinga safari hiyo. Katibu wa masuala ya kimataifa wa COSATU, Bongani Masuku amesema kuwa, siasa za Marekani zimejikita zaidi katika kuzalisha na kukithirisha silaha za nyuklia na kusambaza silaha ulimwenguni, jambo ambalo linavuruga amani, uadilifu, demokrasia na haki za binadamu.
Jumuiya ya Mawakili wa Kiislamu nchini Afrika Kusini imetaka Rais Barack Obama wa Marekani atiwe mbaroni kwa kutenda jinai za kivita. Jumuiya hiyo ya mawakili ime…

AFYA YA MANDELA BADO UTATA-ZUMA AHAIRISHA ZIARA YAKE YA MSUMBIJI

Image
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefutilia mbali ziara yake ya kwenda Musumbiji baada ya kumtembelea hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema kuwa Bwana Mandela yuko katika hali mbali ya afya.
Msemaji wa Zuma Mac Maharaj amesema kuwa hali yake imedorora zaidi katika saa 48 zilizopita.

Afrika Kusini
Mandela ambaye, ni rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.
Madaktari wanasemekana kufanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Mandela anapona.
Vikundi vya watu wenye huzuni mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela, walikusanyika nje ya hospitali alikolazwa, wakiwa na ujumbe wa ugua pole kwa Mandela
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.
"tutasikitika sana ikiwa tutapata habari za kifo chake, lakini pia tutakuwa tunasherehekea maisha yake. Amefanya mambo mengi zaidi kwa nchi yetu,'' alisema kijan…

Dunia ina mambo-MWANAMKE ATUMIA "PERIOD BLOOD"KUFANYIA ART WORK

Image
Chilean artist Carina Úbeda has saved five years’ worth of her own menstrual blood... for the sake of art.

 "I can not wear pads because they trigger an allergic reaction," Úbeda explained to Soy Chile. Instead of tossing her sanitary cloths aside, she decided to save the soiled fabric until inspiration struck.

For her current exhibition at the Center of Culture and Health in Quillota, Chile, entitled "Cloths," the artist put 90 used sanitary rags on display, each embroidered with words like "destroyed" and "production." Each embroidered rag is placed in an embroidery hoop and hung up, surrounded by dangling rotten apples symbolizing ovulation.

While some were disgusted by Úbeda's choice of material, others saw poignancy in the medium. "Male blood is celebrated for being brave while ours is a shame," one visitor told the Daily Mail. "This won't change until we release our body as the first stage of political struggle."…

TATOO ZA WASANII KADHAA WA BONGOMOVIES ZILIZOWEKWA HADHARANI

Image
Baada ya waigizaji kadhaa wa bongo movies kuendelea kuzianika tattoo zao mbalimbali zilizopo kwenye miili yao,sasa ni zamu ya mwigizaji Anyefanya vizuri sana kwenye tasnia ya filamu nchini CHUCHU HANS KICHUNYA kuziweka zake hadharani baada ya jana kuweka picha kadhaa kwenye mtandao zikionesha tattoo hiyo iliyoko maeneo ya kiunoni kwa juu kidogo.

Huyu anakuwa msanii mwingine tena wa bongo movies kuweka wazi tattoo zake baada ya waigizaji waliozoeleka kwenye jamii kwa tattoo zao kama Wema sepetu, Irene Uwoya, Jacquiline Wolper na MaindaMakala- SATELITE YA KWANZA KURUSHWA ANGANI(SPUTNIK)

Image
Ilirushwa Mnamo mwaka 1957
 The Soviet space agency launched Sputnik 1 into orbit to become the first artificial satellite.
 This success is considered the beginning of the Cold War's Space Race between the Soviet Union and the United States.
 The football sized satellite broadcast a radio signal during its 98 minute orbit for 22 days until the batteries ran out.
 Sputnik 1 re-entered the atmosphere and was destroyed on January 4, 1958.MANDELA BADO HALI TETE,MAOMBI ZAIDI YATOLEWA

Image
Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.
Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.
Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee …

"PINDA AWAOMBE RADHI WANANCHI"KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU

Image
Kituo cha sheria na haki za binadamu-LHRC kimemtaka waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda,kuwaomba radhi Watanzania kupitia bunge, kufuatia kauli aliyoitoa hivi karibuni bungeni mjini Dodoma , akiviamuru vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo jeshi la polisi kuwadhibiti wananchi kwa kuwapiga pale wanapo kaidi amri halali inayotolewa na jeshihilo
source ITV

VYUO 100 BORA "UDSM NAFASI YA 6"

Image
Kwa mujibu wa World University Web Ranking hii hapa ndio list ya vyuo 100 Tanzania ikiwa nafasi ya 6 kupitia chuo cha Dar es salaam.South afrika ikiongoza kushika nafasi za juu katika list hiyo.

CHEKI HAPA


1 University of Cape Town- South Africa

2 University of South Africa -South Africa

3 University of Pretoria -South Africa

4 Universiteit Stellenbosch-South Africa

5 University of the Witwatersrand-South Africa

6 University of Dar es Salaam-Tanzania


7 Cairo University-Egypt

8 University of KwaZulu-Natal-South Africa

9 The American University in Cairo-Egypt

10 Makerere University     -Uganda

11 Rhodes University-South Africa

12 University of the Western Cape-South Africa

13 Mansoura University-Egypt

14 University of Johannesburg-South Africa

15 Université Cheikh Anta Diop                -Senegal

16 Assiut University-Egypt

17 University of Nairobi- Kenya

18 Zagazig University-Egypt

19 University of Botswana-Botswana

20 Université Mohammed V – Agdal-Morocco

21 University of Ghana -Ghana

TAMKO LA SERIKALI POLISI KUUWA RAIA

Dar es Salaam.
 Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.

“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.

Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.

Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume…

LOWASA KUGOMBEA URAISI 2015"MAONI YA WANAFUNZI UDOM"

Image
Waziri Mkuu aliyejiuzuru na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Ngoyai Lowasa alipotembelewa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DODOMA (UDOM) ambao walitokea katika shule zasekondari za kata.

Wanafunzi hao, pamoja na kumpongeza Mh. Edward Lowassa kwa kuasisi na kusimamia ujenzi wa shule za sekondari katika ngazi ya kata pia wamemtaka achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia. Pia wameahidi kujichangisha
fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika


UJENZI WA BOMA LA GESI MTWARA-ULINZI MATHUBUTI

CLICK LINK HAPA CHINI KUSOMA HABARI KAMILI
Polisi waimarisha ulinzi kwa wajenzi wa bomba la gesi

NATASHA GET MARRIED SOON

Image
Hatimaye ile ndoa iliyokuwa ikusubiriwa kwa hamu kubwa na ndugu jamaa na marafiki wa mkongwe wa filamu Tanzania Suzan Lewis maarufu kama Natasha imewadia baada ya juzi kufanyiwa sherehe ya “kufundwa” kabla ya kukabidhiwa kwa mumewe hivi karibuni.

Katika habari iliyoripotiwa kwa picha na mtandao wa global publishers sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya  Tandika Maghorofani, Dar ambapo iliandaliwa na rafiki wa karibu  wa Natasha aliyejulikana kwa jina moja tu la Nuru.

Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mastaa wengi mavazi yalionekana kuwa ya kiasili zadi na kina dada hao kuonekana wakikata viuno vya nguvu kumpongeza Natasha

Baada ya yote hayo kukamilika, msafara wa kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo ulianza huku ngoma zikiendelea kupigwa mpaka nyumbani kwa Natasha

Akizungumzia shughuli hiyo, Natasha alisema: “Nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu. Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia.”MAGAZETINI JUMATANO HII

Image

Updates-JOSEPH MBILINYI A.K.A SUGU AACHIWA KWA DHAMANA

Image
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.

Mwandishi wetu akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.

Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.

Hata hivyo taarifa za awali za tukio la kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.


Picha-CECAFA YAINGIA NUSU FAINALI

Image
Mashindano ya kandanda ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ya kuwania kombe la Kagame yameingia nusu fainali nchini Sudan sehemu ya Darfur Kaskazini na Kordofan Kusini.
Jumatano wiki hii Express ya Uganda inapimana nguvu na APR ya Rwanda kisha wenyeji Al Ahly Shandy dhidi ya Al Merreikh ya kutoka El Fashir, mji mdogo ambao una uwanja wa kimataifa wa ndege pamoja na viwanja vya kisasa vya voliboli, mpira wa kikapu na kandanda.
Mechi hiyo ya wenyeji inasubiriwa kwa hamu. Al Merreikh ina mashabiki wengi na wachezaji kadhaa wa nje baadhi yao Joseph Kabagambe ambaye ni mchezaji kutoka Uganda wa kiungo cha kati na Adam Williams wa Nigeria. Mchezaji mwingine wa Nigeria David Nwosu anayechezea Merreikh hatacheza kwa sababu ya kuonyeshwa kadi mbili za manjano..
Alhamisi wiki hii Vital'O ya Burundi inapepetana na Ports ya Djibouti mechi ya kwanza ya robo-fainali, na ya pili ni kati ya Rayon ya Rwanda na URA ya Uganda. Mechi za nusu-fainali ni Ijumaa na Jumamosi kisha Julai tarehe mosi …

WATU 37 WAFARIKI DUNIA KWENYE MGODI

Image
Wachimba migodi 37 wameuawa baada ya mvua kubwa kusababisha kuporomoka kwa machimbo walimokuwa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Maafisa wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea Jumapili karibu na mji wa Ndassima, umbali wa kilomita 440 Mashariki mwa mji mkuu,Bangui.
Taarifa zinazohusiana
afrika magharibi
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, siku tatu za kuomboleza zimetangazwa nchini humo.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ina utajiri wa dhahabu na almasi lakini imekumbwa na mzozo wa muda mrefu, baada ya waasi kupindua serikali mwezi Machi.
Msemaji wa rais Prosper Ndouba, alisema kuwa anahofia kuwa watu zaidi huenda wakafariki.
"kufikia sasa idadi ya waliofariki ni 37, ingawa kuna wengi zaidi waliojeruhiwa, '' alisema bwana Ndouba
Afisaa mmoja ambaye hakutajwa jina aliambia shirika la habari la AFP kuwa idadi kubwa ya wachimbaji walikuwa kwenye machimbo hayo yaliyogeuka na kuwa tope baada ya mvua kubwa kunyesha na hivyo kuwaporomokea


Breaking News-JOSEPH MBILINYI A.K.A SUGU MBARONI

Image
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi amekamatwa kwa kile kinachodaiwa ni uchochezi na kumkashifu Waziri Mkuu Mzengo Pinda.
Hivi  karibuni, Mh. Sugu  alidai  kuwa  Tanzania  haijawahi  kuwa  na  waziri  mkuu  mpumbavu  kama  Mizengo  pinda


WEMA & KAJALA PETE NA KIDOLE

Image
Baada ya siku chache za magazeti ya udaku nchini kuripoti kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa karibu sana kati ya mwanadada Wema sepetu na Muigizaji mwenzake Kajala masanja, tuliamua kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa suala hili ili tusije kuipotosha jamii kwa habari za zisizo na ushahidi wowote.

Katika habari iliyoripotiwa na blogs na magazeti kadhaa ya udaku kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema kuwa chanzo ni vitendo vya mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala kwenye dili anzopata za kucheza filamu na hasahasa kumkosesha dili ya kwenda china kufanya filamu aliyoalikwa na watanzania waishio nchini humo.Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta hewani wasanii hawa ili tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada Kajala alikuwa wa kwanza kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo na kuwashangaa wanaoziandika wanazipata wapi.

“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mku…