(Exclusive)ANGALIA HII VIDEO KWA MAKINI MWANZO MPAKA MWISHIO

Hebu mdau wa blog hii angalia na sikiliza kwa makini maneno ya  huyu dada.
Nawauliza swali...... Je mnamfahamu huyu dada?
Na unamfahamu vipi huyu dada?

Ameamua kutoa duku duku lake la moyoni kwa kitu kilichowahi kumtokea katika maisha yake baada ya dada mmoja kutaka kufanyia usagaji ili kumsaidia.


Chanzo-Mpekuzi blog
Share:

MSANII KENYA "HABIDA" AFIWA NA BABA YAKE

Habida Moloney, Staa wa muziki kutoka Kenya ambaye kwa sasa anatamba kwenye airwaven na ngoma/video yake ya 'Lights Up' yupo katika kipindi kigumu kwa wakati huu baada ya kumpoteza baba yake mzazi wiki hii katika Hospitali ya Aga Khan huko jijini Nairobi Kenya.

Msanii huyu ameamua kuweka maneno yafuatayo katika mtandao kushare hisia zake za upendo pamoja na huzuni kubwa ambayo imempata kwa kuondokewa na baba yake.

“To the greatest Husband, Father, Brother, Grandfather and much more. I love you and miss you dearly. May you rest in peace and may you be right there near the Lord. Good bye daddy”.


Share:

(AFYA LEO)-UGONJWA WA PUMU (ASTHMA)


Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu (inflammation) na kuvimba.

Maumivu katika njia za hewa huzifanya kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda kwenye mapafu. Hali hii husababisha muathirika kutoa mlio kama wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua.

Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu lakini unaotibika. Unaweza kudhibitiwa kama vile ugonjwa wa kisukari na moyo unavyoweza kudhibitiwa.


Aina za Pumu

Kuna aina kuu mbili za pumu. Aina ya kwanza ni ile inayoanza mapema (early onset asthma) na aina ya pili ni ile inayochelewa kuanza (late onset asthma).
Kwa kifupi tutaenda kuangalia tofauti chache kati ya aina hizi za pumu.

Pumu inayoanza mapema
Ni kawaida kwa aina hii ya pumu kuanza utotoni na kwa kawaida huwatokea waathirika ambao miili yao hutengeneza kingamwili (antibodies) za IgE.
Waathirika wa aina hii ya pumu hutambuliwa kwa vipimo maalum vya ngozi ambapo huonesha kuathirika kwa asilimia kubwa vipimo hivyo vinapofanywa.

Pia waathirika hawa huwa na matatizo mengine ya mzio (allergic disorders) kama mafua na ukurutu (eczema).

Pumu inayochelewa kuanza
Aina hii ya pumu tofauti na iliyopita huanza katika umri wowote na asilimia kubwa ya waathirika ni watu wazima. Hakuna ushahidi wowote unaohusianisha vizio (allergens) vinavyotokana na mazingira na uwezo wa kusababisha aina hii ya pumu.

Pumu husababishwa na nini?

Bila shaka mpenzi msomaji umekua ukijiuliza swali hili mara kwa mara. Haifahamiki haswa ni sababu zipi zinazopelekea njia za hewa kupata maumivu na hivyo kupelekea mtu kupata pumu.

Vyanzo mbali mbali vinaonyesha kuwa inatokana na mseto wa vitu kama tumbaku, maradhi na baadhi ya vizio.

Pia kuna vitu katika mazingira ambavyo vinaweza kusababisha mtu kushambuliwa na pumu. Vitu kama vile mazoezi, vizio, viwasho (irritants) na maradhi yatokanayo na virusi.

Baadhi ya vizio ni kama vifuatavyo:
-Vumbi
-Mende
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k

Viwasho kama:
-Moshi wa sigara
-Uchafuzi wa hewa
-Harufu kali (kutoka kwenye rangi au chakula)
-Msongo wa mawazo

Vingine ni kama:
-Dawa kama Aspirin
-Ugonjwa wa kucheua
-Viwasho au vizio vitokanavyo na kemikali
-Magonjwa ya njia ya hewa n.k

Ieleweke kwamba orodha iliyotajwa hapo juu siyo kamilifu kwa maana kwamba haijasheheni vitu vyote vinavyoweza kuleta dalili za pumu na pia muathirika anaweza kuathirika na kimoja wapo au zaidi.

Vigezo hatarishi

Baadhi ya vigezo hatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano wa kusababisha ugonjwa wa pumu ni pamoja na:

-Kuishi katika miji mikubwa, haswa katikati ya mji ambapo huongeza uwezekano wa kukutana na vizio

-Kuvuta hewa iliyo na moshi

-Kemikali zitokanazo na kilimo, dawa za kutengeneza nywele, rangi, vyuma, plastiki au vifaa vya elektroniki

-Kuwa na mzazi mmoja au wawili wenye pumu
-Kuathirika na maradhi ya mfumo wa hewa kama kikohozi na mafua wakati wa utoto.

-Unene wa kupita kiasi (obesity)

-Ugonjwa wa kucheua na kiungulia (Gastro esophageal reflux disease)

Dalili za Pumu

Baadhi ya dalili za kawaida za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo:

-Kikohozi: Mara nyingi kikohozi cha pumu huwa kikali nyakati za usiku au alfajiri na hivyo kumfanya mwathirika kutolala vizuri

-Kutoa sauti ya mfano wa mtu anayepiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua

-Kifua kubana: Mgonjwa husikia kama kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine husikia kama mtu amemkalia kifuani.

-Kukosa hewa: Baadhi hujisikia kama hawawezi kupumua na kukosa hewa ya kutosha inayoingia au kutoka kwenye mapafu.

-Kupumua haraka haraka

Ikumbukwe kwamba si watu wote huwa na dalili zilizokwisha tajwa hapo juu na dalili zaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.

Dalili pia zinatofautiana ukali. Wakati kwa mwingine dalili zinakuwa za wastani, wengine zinakuwa za kukera tu au mbaya kiasi cha kumzuia muathirika kufanya shughuli zake za kila siku.

Vile vile wapo wengine ambao dalili zinakuwa mbaya kiasi cha kuhatarisha maisha. Dalili pia zaweza kutofautiana kwa kipindi zinapotokea.

Wengine hupata dalili mara moja tu kwa mwezi, wengine kila wiki na wengine hupata dalili kila siku.

Hata hivyo iwapo muathirika atapata matibabu sahihi anaweza kuishi na dalili chache au bila dalili kabisa.

Uchunguzi

Kipimo cha muhimu katika uchunguzi iwapo mtu ameathirika na pumu ni kuangalia jinsi mapafu yanavyofanya kazi.

Kipimo hicho kijulikanacho kwa lugha ya kitaalamu kama spirometry hutathmini kiasi cha hewa mtu awezacho kukitoa baada ya kuvuta hewa kwa nguvu na kwa haraka kiasi gani.

Viwango huwa chini ya kawaida iwapo njia za hewa zina maumivu na zimesinyaa. Kipimo hicho cha spirometry pia hutumika kutathmini jinsi mgonjwa wa pumu anavyoendelea kupata nafuu au tatizo kuongezeka.

Hata hivyo kipimo hicho ni kwa ajili ya watoto wenye zaidi ya miaka mitano na watu wazima tu.

Baadhi ya vipimo vingine vinavyoweza kufanywa iwapo kipimo cha spirometry hakitaonesha tatizo ni:

Kipimo cha Kizio (Allergy test)

Husadia kugundua iwapo kuna vizio mbalimbali vinavyoathiri mwili wako.

Kipimo cha Mazoezi

Kugundua iwapo kuna mabadiliko yoyote katika njia ya hewa kutokana na mazoezi.

Kipimo cha Ugonjwa wa Kucheua na Kiungulia

Kipimo hiki ni muhimu pia kutokana na uhusiano uliopo kati ya kiungulia, kucheua na ugonjwa wa pumu.

Kipimo cha Picha ya Mapafu (X-ray)

Kipimo hiki pia hutumika kuona iwapo kuna kitu chochote kilichoziba njia ya hewa au kama kuna maradhi yoyote katika mapafu au moyo.

Kutokana na vipimo daktari wako atapata picha ya ukali wa pumu yako na kukuanzishia tiba muafaka.

Matibabu

Kuna aina mbili za matibabu ya pumu. Moja ni ile ya dharura ili kutoa msaada au nafuu ya haraka. Dawa hizi ni zile zinazosaidia kutanua njia za hewa ambazo zimesinyaa (bronchodilators) pia husaidia kuilainisha misuli ya njia za hewa iliyosinyaa ili iweze kutanuka na kuruhusu hewa ya kutosha kuingia.

Ni vizuri kutumia dawa za kuleta nafuu haraka punde uonapo dalili za pumu zilizoorodheshwa hapo juu.

Aina nyingine ya dawa ni zile za muda mrefu. Aina hizi za dawa hutumiwa mara kwa mara kwa kipindi kirefu kuzuia dalili za pumu na mashambulizi.

Watu wenye pumu isiyoisha wanahitaji matumizi ya dawa ya muda mrefu. Kotikosteroidi za kuvuta (inhaled corticosteroids) ni nzuri kwa aina hii ya pumu.

Matibabu ya pumu kwa watoto

Watoto wenye pumu kama ilivyo kwa watu wazima wanapaswa kumwona daktari kwa matibabu. Watoto walio na umri mdogo wanahitaji uangalizi wa wazazi/walezi ili kudhibiti pumu.

Watoto wenye umri mkubwa wanaweza kujifunza wenyewe jinsi ya kutumia dawa chini ya uangalizi mdogo kutoka kwa wazazi.

Matibabu ya pumu kwa watu wazima
Watu wazima wanaweza kutakiwa kupunguza au kuongeza matumizi ya dawa za pumu kutokana na maradhi mengine waliyonayo.

Dawa kama ya kutibu shinikizo la juu la damu, ugonjwa unaotanua mboni ya jicho na kutatiza kuona (glaucoma), aspirini na dawa za maumivu (non steroidal anti inflammatory drugs) huingiliana na utendaji wa dawa za pumu au zenyewe kusababisha pumu.

Matibabu wakati wa ujauzito

Ni muhimu kudhibiti vyema ugonjwa wa pumu wakati wa mimba kwani iwapo utasababisha kusinyaa kwa njia ya hewa basi waweza kupelekea upungufu wa hewa ya oksijeni kwa mtoto hali ambayo ni hatari kwa mtoto.

Dawa nyingi za pumu hazina madhara kwa kichanga hivyo ni muhimu kuendelea na matibabu wakati wa mimba kuliko kuacha.

Kinga

Njia pekee ya kujikinga na pumu ni kuepuka vizio vinavyoweza kusababisha kuanza kwa dalili za pumu. Waweza fanya hivyo kwa kusafisha nyumba kila wiki kupunguza vumbi.

Pia unatakiwa kuepuka kufanya mazoezi kwenye baridi, epuka moshi wa sigara, dhibiti ugonjwa wa kucheua na kiungulia, epuka kukaa na wanyama na epuka kuishi katika mazingira yenye hewa yenye unyevunyevu.

Ushauri

Jinsi ya kumsaidia mtoto mwenye pumu

-Mpeleke kwa daktari kwa uchunguzi wa mara kwa mara na matibabu.

-Mueleweshe kuhusu pumu na jinsi ya kuidhibiti.

-Mueleweshe ajue vitu vinavyoweza kusababisha yeye kupata dalili za pumu na jinsi ya kuepukana navyo.

-Muepushe na moshi wa sigara kwa kutovuta sigara na kutoruhusu watu kuvuta sigara nyumbani kwako.

-Tafuta jinsi ya kumpunguzia mtoto wako kukutana na vizio kama vumbi, chavua, mende n.k

-Hakikisha anatumia dawa kama inavyotakiwa

-Mhimize kufanya mazoezi ya viungo


                        TIBA  LISHE  YA  UGONJWA  WA  PUMU

Baadhi ya vyakula vinavyoaminika kutoa ahueni na kuwa kama tiba kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja na asali, juisi ya limau, mchanganyiko wa vitunguu swaumu na maziwa na mchangayiko wa mdalasini pamoja na asali. Vyakula hivyo vikiwa sehemu ya mlo wa mgonjwa kila siku, atapata ahueni ya ajabu.Pamoja na kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, mgonjwa wa pumu anatakiwa pia kula kwa kiasi kidogo mlo wenye matunda, mboga za majani na vyakula vingine vitokanavyo na nafaka ambavyo hutoa ‘alikalaini’.

Aidha, wagonjwa wa pumu wanatakiwa kujiepusha na ulaji wa kiasi kikubwa cha wali, sukari, mtindi (yoghurt), unywaji mwingi wa chai, kahawa, pombe na vyakula vote vya kusindika au kwenye makopo.Mgonjwa anashauriwa pia kufanya mazoezi ya kuvuta hewa safi na kuishi katika hali ya hewa isiyo na baridi, kunywa maji mengi mara kwa mara, kufunga kula (fasting) japo mara moja kwa wiki. Kwa kufuata masharti hayo, mgonjwa anaweza kuishi na pumu bila kusumbuliwa wala kutumia dawa kali kwa maisha yake yote.Pia unatakiwa kuepuka kufanya mazoezi kwenye baridi, epuka moshi wa sigara, dhibiti ugonjwa wa kucheua na kiungulia, epuka kukaa na wanyama na epuka kuishi katika mazingira yenye hewa yenye unyevunyevu.
Share:

{Makala}ANGALIA HUU UTABIRI KUPITIA VIDOLE VYA MKONO WAKO



Utabiri wa walioshija kidole kimoja.Tukianza kidole kidogo kikiwa cha kwanza.

1. Kama umeshika kidole kidogo (sayari ya attwarid) basi mwanzo wa mwaka utasafiri mbali na utapata marafiki wengi na safari itakuwa ya kuelekea upande wa mashariki na utaelekea nchi za joto.Kama umeshika kidole hicho hicho na wakati ni jioni basi utapata hasara au ajali ya gari na pia utaibiwa na kukosa kazi.Kifo cha bibi kizee uliyekuwa nae nyumbani.


2. Kama umeshika kidole cha pete au cha kwanza toka kidole kidogo.Hicho ni kidole cha sayari ya jua basi fahamu utashinda uchaguzi,ubunge,utapata vyeo,kurudi kwa mpenzi wa zamani.Katikati ya mwaka utapata uzazi kirahisi kama ulikuwa huzai,watoto zaidi ya wawili na watu watatu waliombali kuregea.


3. Kama umeshika kidole cha kati au cha pili toka kidole kidogo.Hicho ni kidole cha zohal basi mwanzo wa mwaka utaambiwa magonjwa mengi toka kwa jamaa wa kike,hatari kutokea za talaka au kukimbiana na vile vile kuugua ma oparesheni.Utafiwa na mtoto wako mdogo wa kike.Katikati ya mwaka utafunga ndoa au kusimamia ndoa za marafiki mara kwa mara.Utachaguliwa na kupata cheo cha juu,utapata nafasi ya bunge au mali unayogombania.Kama una jamaa yako kiguru basi atashinda na kuongoza na unashauriwa usikiza na yeye.


4. Kama umeshika kidole cha tatu toka kidogo au kidole cha shahada au kidole cha sayari ya mushtara basi utakimbiwa na mume au mke au aliyembali atakukimbia kisha atarudi kati ya sasa na septemba.Wakwe na mashemeji ndio matatizo yako tahadhari nao.


5. Kama umeshika kidole gumba au kidole cha sayari ya Marikh basi dada au wifi au mama mdogo au shemeji ndio watakao vuruga ndoa yako.Kuna jamaa yako wa kike atakaye kosana na mheshimiwa mmoja,chunga kesi kutokea mara kwa mara na ile kesi iliyotokea chunga isiregee.Katikati ya mwaka utasaidiwa na mtu aliyembali kati ya Novemba na Februari,utashinda uchaguzi na kama una mimba basi utazaa watoto wawili wakiume wenye rangi ya baba yao.


6. Kama umeshika chini ya kidole gumba au sehemu ya sayari ya zuhura basi kama wewe ni mwanamuziki utakuwa huru,wanaharakati kushika ndoa nyingi na wageni kukutembelea.Nafasi za kazi kwa wanawake wenye sura ndefu na waume wenye vichwa vya meza.


7. Kama umeshika chini ya kidole kidogo basi kuna mabadiliko ya kikazi,tahadhari kazini na shirikiana na baba kuna mradi wa nyumba.

Source-sheikh abdulazizi mohamed
Share:

Breaking News-MBOWE ASHIKILIWA NA POLISI

Mwenyekiti wa Taifa Chadema na Kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la polisi nchini na kwa sasa yuko chini ya ulinzi mkali sana wa Polisi.



UPDATES
Mwenyekiti Mbowe tayari ameachiwa huru baada ya majadiliano ya kina kati ya Polisi na Mawakili wa Chadema.

Polisi wamekubali mawakili wa Mbowe kujibu kwa maandishi kwanini alisema polisi wanahusika na mlipuko wa Arusha na kisha watafanyia kazi majibu hayo na kutoa uamuzi wao
Share:

DOWNLOAD WIMBO WA QASWIDA WA TUNDA MAN

Kutoka kwa Tunda man

"Nimeandaa album ya qaswida yenye jumla ya nyimbo 6 "TUFUNGENI NA KUSWALI" Kwa sasa nimeachia wimbo ambao umebeba jina la album, unaweza kusikiliza na Kudownload hapa."


Share:

KIWANDA CHA KUTENGENEZA SILAHA TANZANIA CHAGUNDULIKA

Kiwanda cha kienyeji cha kutengeneza vifaa na silaha mbalimbali,kimegundulika kuwepo jijini Dar es Salaam,ambapo wahusika wa kiwanda hicho wamekiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambayo yamesababisha mauaji mengi sehemu mbalimbali. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, kamishna msaidizi wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam DCP Ally Mlege,amesema katika hali ya kushangaza baada ya kukamatwa kwa baadhi ya watuhumiwa waliokuwa wakijihusisha na matukio ya ujambazi,hatimaye baada ya kubanwa na jeshi la polisi walikubali na kusema kiwanda hicho kilichopo maeneo ya Kawe Mzimuni kinatumika katika kutengeneza na kukarabati vifaa na silaha mbalimbali zinazotumika katika matukio ya uporaji na unyang'anyi ambavyo vilitumika na kusabisha mauaji mengi sehemu mbalimbali.
Aidha tapeli hatari bwana Mfaume Omary maarufu kwa jina la Mau(29)mkazi wa Magomeni Kagera,ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kutumia namba tofauti za mitandao ya simu na majina ya watu maarufu ikiwemo viongozi wa serikali na viongozi wa dini kwa lengo la kujipatia fedha kwa kuvaa uhusika wa mtu husika bila wanaombwa fedha hizo kugundua.
Jeshi la polisi limekanusha vikali kuhusu habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuwa mbunge wa jimbo la Ubungo Mh John Mnyika amekoswa na bomu na kumjeruhi moja ya wafuasi wake kuwa ni la huzushi,na ukweli ni kwamba bomu hilo lililipuka ndani ya gari la polisi Pt .1902 wakati askari dcp Julius alipokuwa ndani ya gari akisogeza box lenye mabomu ya machozi na kwa bahati mbaya bomu hilo lililipuka ndani ya gari hilo lakini halikuleta madhara kwa askari polisi yeyote wala raia waliokuwa katika eneo hilo


Share:

ASKARI 117 WAFUKUZWA MAFUNZONI

Wanafunzi 117 wa Polisi, wamefukuzwa katika Chuo cha Taaluma na Mafunzo ya Polisi (MPA), kilichopo Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Waliotupiwa virago na kufutwa kwenye kozi hiyo ni wale waliopoteza sifa za kuendelea na mafunzo ya kijeshi baada ya kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, utoro na matatizo ya kiafya.
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Matanga Mbushi, ambaye ni mkuu wa chuo hicho aliliambia NIPASHE katika mahojiano maalumu kwamba, waliotimuliwa chuoni ni kati ya askari wanafunzi 3,189 waliokuwa wamesajiliwa kuanza mafunzo ya kijeshi katika chuo hicho, Oktoba 25 mwaka jana.
Kati yao askari 115 ni wale wa Polisi na askari wawili wanatoka katika Idara ya Uhamiaji iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Kufukuzwa kwa wanafunzi hao , kuna akisi moja kwa moja jinsi menejimenti ya chuo hicho ilivyojipanga upya kupunguza wimbi la baadhi ya askari walioko kazini na ambao wanalipaka matope jeshi hilo kutokana na kupotoka kimaadili kwa kutaka kujinufaisha kimaslahi.
Askari hao walikuwa waungane na wenzao ambao wanatarajiwa kuhitimu mafunzo ya awali ya polisi na uhamiaji, Julai 26 mwaka huu baada ya kupatiwa mafunzo ya medani za kivita. Mgeni wa heshima atakayeshuhudia kuagwa kwa askari 3,092 ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.
Kamishna Mbushi alisema askari hao pamoja na mambo mengine wamepatiwa mafunzo maalumu ya utunzaji wa amani ya nchi iliyopo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Haki za Binadamu, Masuala ya mtambuka (Cross cutting issues), Usimamizi wa majanga na Usimamizi wa kazi za Polisi.
Mafunzo mengine ni pamoja na Polisi Jamii, Sheria ya ushahidi, Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, Upelelezi wa makosa ya jinai, Usalama barabarani na stadi za kazi.
Taarifa za awali kutoka ndani ya chuo hicho, zinaeleza kuwa mahafali hayo ya Polisi yatatanguliwa na medani za kivita yatakayofanyika Julai 25 huko katika Kijiji cha Kilele-Pori, Wilaya ya Siha


Share: