Je Wajua??? EMANUEL ADEBAYO ALIKUWA AMEPOOZA MIGUU KWA MIAKA 4 TANGU ALIPOZALIWA

Mchezaji machachari Emannuel Adebayo alikuwa ni mtoto ambaye amezaliwa akiwa amepooza miguu na ilisemekana angekuwa mlemavu kabisa.Wazazi wake walihangaika kila kona kutafuta tiba ya maradhi yake bila mafanikio.Ndipo siku moja mpira uliingia katika kanisa alilokuwa akifanyiwa maombi ghafla alinyanyuka na kuukimbilia ndipo alipoanza kutembea .

ANGALIA VIDEO HAPA CHINI

Share:

(Progeria) UGONJWA WA AJABU UNAMFANYA MTU AZEEKE HARAKA

Ugonjwa wa ajabu unaosemekana kuibuka duniani ambao mpaka sasa inakadiriwa watu 80 wameathirika kutokana na ugonjwa huo.Ugonjwa huu unasemekana mtu akiupata huwa unamfanya akue haraka zaidi kuliko kawaida amabapo imekadiriwa mtu mwenye ugonjwa huu ana uwezo wa kukua kwa zaidi ya mara 8 ya umri alionao ina maana kama una miaka 20 zidisha mara 8 utakuwa na miaka 160.
Ugonjwa huu unaitwa PROGERIA ambao mpaka sasa umeadhiri zaidi nchini india.

Kati ya kijana aliyeadhirika na ugonjwa huu ni kijana huyu mwenye miaka 14 ambaye kwako wewe ndugu msomaji na mtembeleaje wa blog hii ukiangalia picha utaona ni kama mtu mwenye miaka 90 mpk 100.
Kijana huyo anayeitwa All Hussain mwenye miaka 14 ndiyo muadhirika wa ugonjwa huo kutoka India ambaye anasema kuwa ana matumaini ya kupona kwakuwa anamini dawa ya ugonjwa huo ipo.Ingawa wazazi wa mtoto huyo wakiwa na hofu ya kumpoteza mtoto wao kwakuwa hapo nyuma waliwapoteza wengine kutokana na ugonjwa huo.



BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI UGONJWA WA AJABU
Share:

SAMAKI SAMAKI YAWAKA MOTO

Baa maarufu iliyopo maeneo ya mbezi beach jiji dar yateketea kwa moto leo mida hii ya mchana kikiwa chanzo cha moto huu mpaka sasa hakijajulikana.
Wananchi wa maeneo ya karibu wanajaribu kudhibiti hali hiyo ambayo mpaka sasa imedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.


Share:

NEY WA MITEGO & CHID BENZ SASA BIFU HAKUNA

Inajulikana bifu zito linaloendelea kati ya hawa wakali wawili lakini kwa sasa limefikia ukingoni baada ya madee kufanya kitu fulani na kuwaunganisha wakali hao wakati wakipiga show ya fiesta mjini SINGIDA hivi karibuni.

HABARI KAMILI BOFYA HAPA CHINI

NEY & CHID BENZ NO BEEF



Share:

(Picha)HII NDIYO NIGHT CLUB MPYA JIJINI-CLUB LITE

Ikiwa tasnia ya kufanya starehe kushika kasi jijini dar,sasa kumefunguliwa kiwanja kipya kabisa.Club yenye mazingira mazuri sana ambayo imejengwa kwa ustadi wa hali ya juu sana.Ingawa eneo ilipo ni mahala ambapo mtu huwezi kuamini kama panaweza kuwepo night club nzuri namna hii kama mimi mwandishi nilivyoiona.
Jina la club hiyo likiwa limetokana na bia maalufu sana ya CASTLE LITE,Ndipo club hiyo ikapewa jina la CLUB LITE.Najua wengi wetu tunajua maana ya neno LITE basi ndivyo hivyo hivyo club hiyo ilivyo kutokana na muonekano wake pia burudani inayopatikana hapo.

ENEO ILIPO.
Club lite inapatikana kigogo karibu na kigogo police post ndani ya baa maalUfu kigogo  nzima yaani NEW PALM VIEW BAR ama wengine huita BAA MPYA.

RATIBA YA BURUDANI.
INAANZIA ............JUMA5-  WANAUME & WANAWAKE - 5000 Wakati nje ya baa kuna baikoko


                             ALHAMISI & JUMAPILI - WANAWAKE BURE
                                                                   - WANAUME 5000


                              IJUMAA & JUMAMOSI-WANAWAKE & WANAUME 5000

Inategemewa kuwekwa siku wanaume bure yaani gentlmen FREE.

HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA MUONEKANO WA NDANI WA CLUB LITE


Share:

MSICHANA ACHAPWA VIBOKO KWA KUVAA NUSU UCHI

Mmomonyoko wa maadili unazidi kuangamiza vijana hasa watoto wa kike.Mapema hii leo jijini arusha msichana ajikuta akichapwa viboko kisa ni nguo fupi aliyokuwa amevaa.Watu wanaopenda kuendeleza maadili ya jamii walilikosoa jambo hilo na kuamua kumchapa viboko msichana huyo.

HABARI KAMILI BOFYA HAPA KUTOKA ITV

MSICHANA ACHAPWA VIBOKO



Share:

POLISI WATAWANYA WAANDAMANAJI-MOROGORO

Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limezima maandamano na kuwatawanya kwa mabovu ya machozi na risasi za mipira wakulima wa vijiji vya kisara tarafa ya Turiani wilayani Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wakipinga wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima .


Malalamiko hayo ya wakulima yamekuja kufuatia tukio la ngombe za wafugaji kuuawa ambapo wakulima hao wametupia lawama jeshi la polisi kushindwa kuondoa mifugo katika maeneo ya wakulima kama ilivyoagizwa na serikali ya wilaya na kuwatuhumu askari kutumia nguvu kutawanya maandamano na baadhi ya wakulima kushikiliwa na jeshi la polisi.

Akizungumzia tuhuma hizo mkuu wa kituo cha polisi Turia Rajab Shemndolwa amesema wamelazimika kutumia nguvu kutokana na wananchi kutofuata taratibu za kufanya maandano na kukaidi amri ya jeshi na kwa kufunga barabara kwa mawe kwa zaidi ya masaa manne na kuzuia shughuli za usafiri.

Nae mkuu wa wilaya ya Mvomero Antony Mtaka akizungumzia tuki hilo amekiri uharibifu mkubwa uliofanywa baada ya mahindi kuliwa na mifugo hali inayosababisha njaa kwa wakulima waliolima lakini kuwa mkakati wa serikali sasa ni kusikiliza malamiko ya pande zote mbili katika kutatua mgogoro huo.
Share:

MUGABE KUAPISHWA LEO

Rais wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe, anaapishwa rasmi leo kwa awamu ya saba kama kiongozi wa taifa hilo, ikiwa ni siku chache baada ya mahakama nchini humo kuthibitisha matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 31 mwezi uliopita, ambao matokeo yake yalipingwa na mpinzani wake, Morgan Tsvangirai. Chama cha Tsvangirai, cha Movement for Democratic Change, MDC, kitasusia sherehe ya kuapishwa kwa Mugabe katika uwanja wa mpira mjini Harare.


Share:

WADADA IGENI HII YA JOKATE

Mrembo anayefanya vizuri katika mambo mengi sana nchini Jokate Mwegelo amezungumza na kutaja Mambo manne yanayomfanya apendwe sana na wanaume wengi hapa nchini.

1. Kujiamini

Hii ndi sababu kubwa ya kwanza aliyoitaja jokate. Ansema hamna kitu kinachowavutia watu, hasa wananume kama kujiamini. Mwanaume anapenda msichana anayejiamini. Zaidi ya yote hamna kitu kinachosema kuwa “I’m sexy” Zaidi ya mwanamke anayejiamini

2. Kujitegemea

Hii ni kama sababu ya kwanza hapo juu,  Jokate anasema hamna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vya kwako basi jua atakupenda sana

3. Kupendeza

Jokate anasema ni muhimu kwa wadada kuvaa nguo nzuri ambazo zitakupendeza kulingana na mwili wako hasa hasa nguo zenye rangi ya kuonekana.

4. Tabasamu

Tabasamu kila saa kwani tabasamu linakufanya unaonekana mzuri Zaidi.




Wachunguzi wa mambo wamesema kuwa sababu hizi ndio pia zilichangia Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Diamond platnumz kumpenda mwanadada huyu kwani sifa hizi hazipo kwa wadada wengi wa mjini
Share:

HIKI NDIO KIWANJA CHA KURUKA KILA IJUMAA NA JUMAMOSI

Hii ni club inayomilikiwa na mhindi ambaye aliamua kuwekeza maeneo ya Mbezi beach.Club hii aliyoamua kuipa jina la Ambrosia Bistro n Bar  kutokana na kwamba mmiliki wa eneo hilo ndiyo yule wa zamani aliyekuwa na garden bistro kama unakumbuka.

Hii aliyoijenga ,maeneo ya mbezi beach kwa wale wanaopitia njia ya tegeta wanashuka kituo cha Afrikana kisha unachukua bajaji unamwambia akulete eneo hilo almaaarufu kama BAA YA WAHINDI.
Na wale wanaopitia njia ya kawe wanashuka kituo cha maringo kisha utakuta bajaji zinaenda eneo linaloitwa KWA ZENA unashuka mwisho hapo kwa zena kisha unafuata barabara mbele kidogo utaiona hiyo Ambrosia Bistro

RATIBA YA BURUDANI

Ijumaa na jumamosi na siku zote za sikukuu disko kabambe linapigwa hapo mpaka asubuhi.

KIINGILIO

Siku hizo za disko kiingilio kinakuwa bure kwa wale watakaofika kabla ya saa 4 na kusubiri disko lianze huku wakipata moja moto moja baridi.
Baada ya saa 4 disko likianza kiingilio ni 10000 tu.

WOTE MNAKARIBISHWA.


mAWASILIANO ZIDI 0779 585858





Hali inakuwaga hivi siku za ijumaa na jumamosi
Share:

FEZZA KESSY NA ONEAL KITAELEKA TU

Baada ya kukutana big brother na kuchipua  penzi kati ya kijana wa botswana Mr Oneal na Mrembo kutoka Tanzania Fezza Kessy,sasa penzi hilo limefika patamu baada ya mwanadada huyo kutolewa mjengoni na kurudi TZ siku chache zilizopita,na hivi karibuni ameamua kumfuata mchizi huko alipo kwao Botswana.
Pamoja na yote Feza amekuwa akitupia tweet kadhaa mtandaoni zikionyesha kuzimika kinoma na mchizi huyo wa Botswana.

Ama kweli penzi la dhati halijalishi umbali ulipo utalitafuta mpaka upate.



PICHANI FEZA AKIWA NYUMBANI KWA KINA ONEAL BOTSWANA
Share:

HAWA NDIO WAANZILISHI WA "WHATSAPP"


Whatsapp ni application wa kutuma messeji ambayo imetengezwa mnamo mwaka 2009 na watu wawili ambao ni  Brian Acton na Jan Koum.

Inasemekana hawa jamaa ni veterani wa yahoo mjini califonia.

Mpaka kufikia mwezi Augusti mwaka 2013 whatsapp imekuwa na watumiaji 300 million zaidi,na picha 325 million zimekuwa shared kupitia mtandao huo wa kijamii.

 Jan Koum
Brian Acton
Share:

WAHAMIAJI HARAMU KURUDISHWA KWAO

Serikali ya Tanzania  imefafanua zoezi la Serikali hiyo la kutaka kuwaondoa wahamiaji haramu walioko katika mikoa mbalimbali ya pembezoni mwa nchi hiyo ya  Kagera, Kigoma na Geita.
Jumanne jijini Dar es salaam Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dakta Emanuel Nchimbi ambaye wizara yake inahusika na idara ya uhamiaji ametoa taarifa ya zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu katika mkutano na waandishi wa habari.

Waziri Nchimbi kwanza alitoa ufafanuzi wa wahamiaji hao haramu ili kuondoa mkanganyiko unaoenezwa kwamba Tanzania imeamua kufukuza raia wa mataifa jirani.

Alisema wanaotakiwa kuondoka ni wale wanaoishi nchini kinyume na sheria ya uhamiaji inayowataka kuomba vibali maalum vya ukaazi na ufanyaji kazi hapa nchini

Kuna madai pia kwamba wahamiaji haramu walioamua kuondoka kwa hiari yao baada ya agizo la mkuu wa nchi Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, hawatendewi haki wengi wanaporwa mali zao na kufanyiwa uhuni.

Waziri wa mambo ya ndani amesema kufanya hivyo ni kosa kisheria na ndiyo sababu wametoa agizo la wahamiaji wanaotaka kuondoka na mali zao watoe taarifa kwa vyombo vya usalama ili polisi wawasindikize mpaka mpakani.

Wahamiaji haramu 10,672 wameshaondoka nchini Tanzania kuanzia kutangazwa kwa operesheni hiyo na Rais mwishoni mwa mwezi julai mwaka huu.
Ripoti ya Dina Chahali


Wahamiaji haramu waliorejea makwao kutoka nchini Tanzania  ni kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Tatizo la Wahamiaji haramu limekuwa kubwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Serikali imeahidi kuendesha operesheni ya kushtukiza wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili  ya  kuwarejesha kwa nguvu wahamiaji haramu wote waliopo kwenye maeneo mbalimbali nchini


Share:

INASEMEKANA KIONGOZI WA BOKO HARAM AMEKUFA

Huenda kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigera, Abubakar Shekau aliuawa na maafisa wa usalama katika ufyatulianaji wa risasi. Duru za kijeshi zinasema huenda Shekau aliuawa kati ya Julai 25 na Agosti 3.
Kundi la Boko Haram ambalo limekua likiendesha maasi Kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka wa 2009 halijatoa taarifa yeyote. Marekani ilitangaza tuzo ya dola Milioni saba kwa yeyote yule angepeana taarifa za kumnasa Shekau.
Taarifa za kijasusi zinasema Shekau alipigwa risasi Juni 30 wakati jeshi la Nigeria liliposhambulia maficho ya Boko Haram katika msitu wa Sambisa Kaskazini Mashariki mwa nchi.
Shekau alipata majeraha mabaya na kuvukishwa hadi katika mji ulioko mpaka na Cameroon kwa matibabu. Inaaminika alikufa kati ya Julai 25 na Agosti tatu mwaka huu. Waandishi wa habari wamesema hakuna taarifa huru ambazo zimethibitisha kifo cha Shekau.
Maelfu ya raia wameuawa tangu Boko Haram kaunza maasi mwaka 2009. Abubakar Shekau alichukua uwongozi wa wapiganaji hao wa kiisilamu baada ya kifo cha mwanzilishi wa Boko Haram, Muhammad Yusuf aliyefariki dunia wakati akiwa kizuizini.
Kundi hilo limeendesha mashambulizi mabaya na ya kikatili wakati wa uwongozi wa Shekau. Boko Haram wamekuwa wakishinikiza kuunda taifa la Kiisilamu nchini Nigeria.
Hapo mwezi Mei mwaka huu Rais Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu Kaskaizni mwa Nigeria ambapo pia alituma jeshi kuendesha operesheni dhidi ya wapiganaji hao.



Abubakar Shekau amekua kiongozi wa Boko Haram tangu mwaka wa 2009. Kundi lake limeendesha mashambulizi ya mabomu na utekaji nyara wa raia.


Share:

HII NDIO MAANA YA "BONGO-BONGO LAND"

Chama cha kibinfasi cha kisiasa cha MEP nchini Uingereza kimeshutumiwa kwa kutumia neno.......'Bongo Bongo Land
Lakini kwa baadhi ya watu nchini Tanzania, neno hilo lina maana isiyo na ubaya wowote.
Mwanachama wa chama hicho, Godfrey Bloom, amenukuliwa kwenye jarida la Guardian akisema,'' inawezekanaje tunatoa msaada wa pauni bilioni moja kila mwezi, kwa 'Bongo Bongo Land' wakati tunakabiliwa na deni kubwa kama hili?''
'Bongo Bongo land' ni neno ambalo hutumiwa miongoni mwa waingereza kama lugha ya dharau kuashiria nchi maskini, au mataifa yanayostawi.
Bloom aliambia BBC kuwa Bongo Bongo Land ni neno wanalotumia watu kuashiria nchi maskini isiyo na ustaarabu.
Hili bila shaka halikumfurahisha Laura Pidcock, mwanaharakati anayepinga ubaguzi wa rangi aliyesema kuwa dhana hizi ambazo watu wanazo kuhusu watu fulani, inarejesha Uingereza nyuma wakati inajipa sifa ya kuwa nchi yenye ustaarabu.
Alisema dhana kama hizo zinapotosha sana.
Wakereketwa wamemtaka kukoma kabisa kutumia tena lugha kama hiyo wakisema kuwa watu katika mataifa ya kigeni watatizama hilo kama ubaguzi wa rangi.
Haya yote yatakuwa habari muhimu kwa watanzania ambako neno hili kwa kifupi,Bongoland lina maana tofauti kabisa na ilivyotafsiriwa na mwanasiasa huyo.
Badala yake inamaanisha mahala ambapo watu wanapaswa kuwa wajanja na kuwa makini wakati wote.
Sehemu hiyo, ni mji mkubwa wa Dar es Salaam. Linatokana na mchanganyiko wa neno la Kiswahili Ubongo - lenye maana Akili,
na neno - land.
Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau anafafanua . "Dar es Salaam ni sehemu ambapo watu hawana budi ila kutumia akili zao. Unaweza kuwa tapeli au mfanyabiashara lakini lazima wawe na mbinu ya kupata pesa.''
Neno hili unaweza kusema ni jipya...kulingana na Famau...limekuwa likitumika kwa miaka 15 sasa. Babake hawezi kuwa analitumia , linatumika sana miongini wa vijana walio chini ya umri wa miaka 35. Lakini linasifika sana kiasi cha kuwahi kuwa jina la filamu iliyotolewa mwaka 2003 kuhusu kijana mmoja mtanzania kuhamia Marekani na fimalu hiyo ikawa na sehemu yake ya pili kwa Bongoland II.
Cha mno zaidi, ikiwa utatumia neno Bongoland nchini Tanzania basi unakuwa umegonga ndipo na kwa hilo unapata pointi hapo wala sio kukosolewa,'' anasema Famau.
Labda ufafanuzi huo ungemsaidia bwana Bloom kujizuia na utata aliosababisha

Godfrey Bloom
Share:

Breaking news-VURUGU MWANZA-MBUNGE ASHIKILIWA NA POLISI

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia kwa mahojiano Mbunge wa Nyamagana jijini humo,Mh Ezekiel Wenje kwa madai ya kuongoza maandamano yaliyosambaratishwa na polisihapo jana kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi


Share:

HUYU NDIO MCHUMBA WA MKALI WA " DAMI DURO" DAVIDO

Kama ulikuwa hujui mkali anaetamba kwa sasa na ngoma kadhaa kama vile GOBE na DAMI DURO anaejulikana kama DAVIDO ndiy msanii au mwanamuziki anaemiliki kifaa hiki hapa kama DEMU WAKE (MCHUMBA WAKE) anayejulikana kwa jina la Funmi Aboderin

Share: