Posts

Showing posts from September, 2013

MSANII AHUKUMIWA MIEZI 6 KWA KUIMBA MATUSI

Image
Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben Ahmed, anayejulikana kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela kwa miezi sita kwa kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa muziki wake. Mahakama ilitupilia mbali kesi yake ya rufaa baada ya yeye na mwanamuziki mwenzake kupatikana na hatia mwezi jana ya kuwatusi maafisa wakuu katika tamasha la muziki eneo la Hammamet. Wawili hao awali walihukumiwa bila ya wao kuwepo mahakamani kutumikia kifungo cha miezi 21 lakini hukumu hiyo iliondolewa. Weld El 15, aliyepatikana na kosa kwa kuimba wimbo wake huo, kuwa 'Ploisi ni Mbwa', hakukata rufaa na sasa yuko mbioni. Hata hivyo Kaly BBJ lisema kuwa wimbo wao ulikuwa unaelezea hali ilivyo nchini Tunisia na kuhusu serikali. Muungano wa vyama unaoongozwa na chama cha wanasiasa waisilamu wenye msimamo wa kadri, Ennahda, uliingia mamlakani baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa rais Zine el-Abidine Ben Ali mwezi Januari mwaka 2011 na uchaguzi kufanyika baadaye mwaka huo…

ALIYEONGOZA SHAMBULIZI KENYA KUINGIA ORODHA YA KUSAKWA ZAIDI DUNIANI

Image
Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.
Bi Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya shambulizi la kujitoa mhanga mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka 2005
Anajulikana kama "white widow", na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wa Interpol hata hivyo hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi lililowaua watu 67.
Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab ilikiri kufanya mashambulizi hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la Westgate na kisha kutekwa kwa raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Kwa mujibu wa polisi wa Interpol, mwanam…

SHAMBULIZI LINGINE KENYA

Image
Kuna taarifa za kikundi cha magaidi wa Al-Shabab kuvamia kituo cha polisi katika mji mdogo wa Mandera uliopo mpakani mwa Kenya na Somalia.

Shambulizi hilo ambalo limefanyika mapema leo limesababisha vifo vya polisi wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa, huku magaidi hao wakichoma moto magari 11.

Duru za kiuchunguzi zinaonesha kwamba hiyo ni sehemu ya mfululizo wa mashambulizi yaliyoandaliwa na Al-Shabab baada ya lile la Westgate, jijini Nairobi.

MATEKA 137 WADAIWA KUUWAWA NA AL SHABAAB

Image
Kundi la Al-Shabaab limedai siku ya Jumatano kuwa mateka 137 waliowachukua wamekufa katika uvamizi wa kituo cha biashara, idadi ambayo ni vigumu kuithibitisha na kubwa kuliko idadi iliyotangazwa kuwa hawajulikani walipo.

Wapiganaji hao walio na mafungamano na mtandao wa Al-Qaeda, katika ujumbe waliouweka katika mtandao wa kijamii wa twitter, walisema mateka 137 waliokuwa wanashikiliwa na mujahedeen walikufa. Waliwashtumu pia wanajeshi wa Kenya kwa kutumia vifaa vya kemikali kukomesha mkwamo huo uliodumu kwa siku nne. "Katika hatua ya uoga wa dhahiri, vikosi vya Kenya kwa maksudi vilitumia vilipuzi vilivyokuwa na kemikali," ulisema ujumbe mmoja na kuongeza kuwa, "ili kufunika uhalifu wao, serikali ya Kenya iliendesha zoezi la kuliporomosha jengo, na kuuzika ushahidi na mateka wote chini ya vifusi."
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alitangaza kumalizika kwa umwagaji huo wa damu uliodumu kwa saa 80 jioni ya Jumanne, ambao ulisababisha vifo vya raia 61 na maafisa sita wa…

HIVI NDIVYO PANYA WANAVYOTUMIKA KUGUNDUA MABOMU ARDHINI

Image
Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania .Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa. Hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi,hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.


Panya wanafundishwa jinsi ya kunusa wakiwa wadogo, kwa kuwekewa vitu vyenye madini ya milipuko.Tangu mwaka 2000, APOPO imekuwa ikiwafunza panya kwenye chuo cha Sokoine,Morogoro. Mwaka 2006 panya wa hao walianza zoezi la kutafuta mabomu ya ardhini huko Msumbiji. Kabla ya panya kuanza kazi ya kunusa wapi mabomu yalipo, lazima wafuzu mtihani kutimiza viwango vya kimataifa vya kutambua mabomu ardhini.


Panya hujifunza kufuata eneo fulani hatua kwa hatua. Waya au kamba hufungwa mwilini kutoka kwenye ufito. Wasimamizi wawili husimama kila upande wa ufito na kumruhusu panya kutembea toka mwanzo wa ufito hadi upande …

ANGALIA SHULE INAYOJENGWA JUU YA MAJI

Image
Watoto katika wilaya ya Makoko laazima wajifunze kuogelea ikiwa wanataka kwenda shuleni. Kwa sababu wilaya hiyo katikati mwa mji mkuu wa Nigeria Lagos imekumbwa na mafuriko tangu mwezi Machi 2013. Shule inayoelea ni mfano wa usanifu majengo wa kiafrika "Afritecture". Usanifu huu unaweka kando dhana za ujenzi wa kimagharibi na kutegemea zaidi mbinu za kienyeji na vifaa kama vile mbao.


(SOMA) MWANADADA ASIMULIA ALIVYOJIOKOA KUTOKA WEST GATE

Image
Sneha Kothari Mashru ni mwanadada mtangazaji wa redio ambaye alikuwa ndani ya jengo wakati tukio linatokea.Asimulia jinsi alivyojiokoa kutoka ndani ya jengo hilo wakati kijana aliyekuwa karibu nae akiwa amepigwa risasi na kufariki.

Asimulia kuwa alitumia damu za watu waliojeruhiwa na waliokufa kujipaka mwilini mwake ili kuonyesha magaidi kuwa na yeye ni moja ya watu walioaga dunia ndani ya jengo.

Kitu cha kwanza alizima simu yake ili isiweze kutoa sauti ikiwa itatokea kuita ili kutowashitua magaidi na kupelekea kupoteza maisha yake.

SOMA HAPA CHINI ALIVYOELEZEA.....

"I realised he was shot, because he was bleeding," she said.

"So I pulled out (his) phone slowly and I tried to switch it off, it was all full of blood, and I tried to switch off the phone so that it could stop ringing (in case it alerted the attackers).

"So I took a lot of his blood, (as) much (as) I could and I tried to put it on myself. I put it on my arm, a lot of the teenager's blood, and while…

MWANDISHI WA VITABU,MTANGAZAJI, MPWA WA KENYATA,MFANYAKAZI WA BENKI YA BARODA WAFARIKI KATIKA SHAMBULIZI

Image
Takriban watu 62 wameuawa kwenye mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya dhidi ya jengo la kifahari lenye maduka zaidi ya themanini la Westgate.


Ruhila Adatia-Sood


Ruhila Adatia-Sood na mumewe Ketan Sood Ruhila Adatia-Sood walioana tu mwezi Januari mwaka jana.
Ruhila, alikuwa katika ghorofa ya juu ya duka la Westgate ambako alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wameandaa mashindano ya upishi kwa watoto.
Alikuwa ameolewa na Ketan Sood, aliyefanya kazi na shirika la USAid mjini Nairobi mwezi Januari mwaka 2012,na harusi yake ilitajwa kuwa harusi ya kiswahili ambayo ilisherehekewa kwa siku tatu.
Alikuwa mjamzito na mimba ya miezi sita alipofariki.
Kulingana na ripoti Adatia-Sood alikimbizwa hospitalini , lakini alifariki baada ya kuwasili kutokana na kuvuja damu nyingi.
Alisifika kote nchini kwa moyo wake mzuri wa kuwafanya watu kutabasamu daima.

Polisi wakikabiliana na wanamgambo hao waliokuwa wameteka jengo la Westgate
Kwenye ukurasa wake wa Twitter alijitaja kuwa mpenda chakula na mtu mweny…

BINGWA WA NGUMI(MASUMBWI) AFARIKI DUNIA

Image
Bingwa wa zamani wa dunia katika ndondi uzani wa Heavyweight mmarekani Ken Norton amefariki akiwa na umri wa miaka 70
Anakumbukwa zaidi kuwa kumshinda gwiji wa masumbwi Mohammad Ali mwaka 1973.
Sawa na mabondia wengi wa uzani mkubwa enzi zake, Ken Norton anakumbukwa kwa jinsi alivyopigana na Mohamed Ali.
Na kwenye pigano lao la kwanza la mwaka 1973, Norton ambaye hadi wakati huo hakujulikana sana alimkomesha Ali na kumshinikiza makonde tangu mwanzo hadi mwisho.
Norton alivunja taya la Ali kwenye pigano la raundi 12, akawa bondia wa pili kumshinda Mohamed Ali tangu alipoanza ndondi za kulipwa.
Katika mapigano yaliyofuatia, baadaye mwaka huo wa 73, Ali alilipiza na kumshinda Norton, na TENA mara nyingine miaka mitatu baadaye kwenye pigano lao la mwisho katika uwanja wa Yankees, mjini New York. Lakini hata hivyo Norton baadaye alitwaa taji la ulimwengu la WBC, kabla ya kulipoteza kwa Larry Holmes mwaka 1978.
Norton, bingwa wa Marekani uzani wa Heavyweith alikuwa ameanza mchezo wa ndoni …

HUYU MWANAMKE MUINGEREZA ASHIRIKI KUSHAMBULIA WESTGATE

Image
Samantha Lewthwaite N i mwanamke mwenye asili ya uingereza ambaye ametajwa kuhusika na shambulio la westgate nchini kenya mapema wiki hii.Huyu ni mwanamke mjane ambaye inasemekana yupo East Afrika na alikuwa anatafutwa na askari Wa kenya kwa kupanga mashambulizi kadhaa ambayo alijaribu kufanya katika nchi kadhaa za mwambao.(coast country)


MAGAIDI 3 WAUWA,ASKALI 11 WA KENYA WAMEJERUHIWA

Image
Taarifa za hivi karibuni kutoka kwa msemaji wa jeshi la kenya KDF zinasema kuwa askali 3 wanaosadikiwa kuwa ni magaidi wameuwa na jeshi lake.Pia ametoa taarifa kuwepo kwa majeruhi 11 wa jeshi lake KDF.

Aliongeza tena kutoa takwimu za watu waliookolewa kutoka katika jengo hilo ambao idadi yake hakuitaja kamili zaidi alisema ni zaidi ya 62.


Raia 11 wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi,huku milio ya risasi ikiendelea kusikika katika eneo la tukio.


"Kenya Defence Forces ( KDF) has reported that three terrorists have been killed and 11 Kenyan soldiers injured in the Westgate operation that has lasted for over 48 hours"


ANGALIA VIDEO JINSI MOSHI NA MILIO YA RISASI HUKO KENYA

(Picha) MOSHI UKIWA UNATOKA KATIKA JENGO LA WEST GATE

Image
Mchana wa leo eneo la West gate kumeonekana moshi mzito ukiwa unavuka kutokea ndani ya jengo lililoshambuliwa jana na kikundi cha kigaidi cha Al shabaab nchini kenya.Kwa mujibu wa BBC wanasema wanajeshi wa Kenya walilipua mabomu  ili kuendelea kukabiliana na tukio hilo.Pia mpaka sasa inasemekana watu waliofariki yafikia 69 na na wengine mamia wamejeruhiwa huku idadi isiyojulikana wakiwa wameshikiliwa mateka na Al Shabaab!!HII NDIYO SABABU YA AL SHABAAB KUPIGA WESTGATE

Image
Katika mahojiano yaliyofanyika hivi karibuni baada ya tukio la mashambulizi nchini Kenya katika sehemu ya kibiashara ya westgate mall,kiongozi wa al shabaab amesema sababu za wao kuamua kushambulia eneo hilo.

".....ni kwa sababu sehemu hii inaingiza pesa nyingi na ipo katikati ya jiji.Ni sehemu wanasikia maumivu na tulitaka ujumbe ufike......."


HILI NDILO JENGO LILILOSHAMBULIWA NA AL SHABAAB NCHINI KENYA

POST HII YA NEY WA MITEGO YALETA UTATA

Hii ni post ambayo imepata comment nyingi ikiuliza kuwa amepata msiba wa nani?


Post by Nay wamitego.

AL SHABAAB WAJITAJA KUHUSIKA NA SHAMBULIZI KENYA

Image
Afisaa mmoja mkuu wa kundi la kigaidi la Alshabaab, amefahamisha BBC kuwa kundi hilo ndilo limehusika na shambulizi dhidi ya duka la kifahari la Westage mjini Nairobi Kenya.
Kwa mujibu wa Afisaa huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita vya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.
Wanajeshi wa Kenya wamekuwa nchini humo tangu mwaka 2011 kama sehemu ya juhudi za muungano wa Afrika kutaka kurejesha uthabiti nchini Somalia.
Afisaa mkuu wa mambo ya ndani Kenya amesema idadi ya waliofariki ni kumi na moja lakini shirika la msalaba mwekundu linasema idadi hiyo imefika watu 30 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa.
Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.

Baadhi ya watu waliofanikiwa kukimbilia usalama wao
Wanamgambo wa Al Shabaab kupitia kwa mtandao wao wa Twitter , wanasema kuwa Kenya haikuchukulia kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka…

WAISLAM WAPINGA MISS WORLD KUFANYIKA INDONESIA

Image
Waislamu kutoka nchini Indonesia wamepiga vita kufanyika mashindano ya dunia ya urembo nchini humo.Kikundi kimoja cha kiislamu kinachoitwa  Indonesian hard line Islamic group kilifanya maandamano makubwa kupinga swala hilo kufanyika ndani ya nchi hiyo na kukiita kitendo hicho kuwa ni ukafiri.
Maandamano hayo yamefanya kuhairishwa kwa mashindano hayo kufanyika Jarkata nchini humo na kutarajiwa kufanyika BALI nje kidogo ya mji wa Jarkata mwishoni mwa mwezi huu tarehe 28/9/.
ROBIN VAN PERSIE- "NAPENDA KUSIKILIZA NYIMBO ZA P SQUARE"

Image
Mshambuliaji machachali wa Manchester United,Robin Van Persie amesema kuwa kati ya vitu anavyopenda wakati akiwa nyumbani kapumzika ni kusikiliza muziki.Alipoulizwa ni aina gani ya muziki ambao anapenda kusikiliza,moja ya watu aliowataja ni wanamuziki kutoka nigeria P Square

Nukuu  alijibu hivi

 “I like to listen to music. ..all sorts honestly. I can listen to Dutch songs, English songs..whatever…if the tune is good I like it… Michael Jackson, Usher, P-Square…all sorts honestly.”
BREAKING NEWS - ELBORU SEKONDARI YAFUNGWA

Shule ya Sekondari Ilboru, imefungwa na serikali kufuatia tishio la kuchomwa moto, kutokana na mgogoro wa wanafunzi na waalimu. Wanafunzi 4 wanahojiwa, 800 wamerudishwa nyumbani

(PICHA) WILLIAM RUTO AKIWASILI MAHAKAMA YA KIMATAIFA

Image
Ile kesi inayokabili makamu wa raisi wa Kenya bwana william Ruto inaendelea kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC.
Deputy President Wiliam Ruto is welcomed to ICC in the Hague by his lawyer Karim Khan. The case had been adjourned.