KIKWETE AUDHURIA MSIBA WA SEPETU

Leo hii rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria msiba wa Balozi Abrahamu Sepetu (Baba mzazi wa Wema Sepetu) uliotokea hapo juzi jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa kiwete amefika msibani akiongozana na mkewe hapo kutoa pole kwa familia hiyo kwa  kuondokewa na Balozi Sepetu ambaye hapo alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye serikali nchini ikiwemo ya kuwa waziri wa mambo ya nje kwenye miaka ya sabini (70) kabla  ya kuwa balozi wa urusi kwenye kipindi cha miaka ya 80. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.





Share:

WAANDISHI WA HABARI WAONYWA-KENYA

Wakuu wa idara ya Polisi nchini Kenya wamewaonya waandisi wa habari kuhusu walivyoripoti matukio katika jumba la Westgate ambako magaidi walishambulia zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Onyo hili linakuja baada ya taarifa za wanajeshi kufanya uporaji katika jengo hilo wakati wakipambana na magaidi hao waliokuwa wamewateka nyara watu waliokuweme ndani ya jumba hili
Mkuu wa polisi, David Kimaiyo alisema kuwa waandishi hawapaswi kutoa kuchochea Propaganda, au kuwachochea wakenya wakati wakipeperusha matangazo yao.
Duru zinasema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamehojiwa na polisi hii leo.
Picha za CCTV zilizofichuliwa kwa waandishi wa habari zilionyesha wanajeshi wakitoka ndani ya jumba hilo na mifuko ya plastiki zilizoshukiwa kuwa na bidhaa kutoka katika mojawapo ya maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya jengo hilo la Nakumatt.
Hata hivyo jeshi limekanusha madai hayo na kusema kuwa wanajeshi walikuwa wanachukua maji ya kunywa wakati wa operesheni yao dhidi ya magaidi.
Takriban watu 67 walifariki ikiwemo wanajeshi na mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo liliosababishwa na Al Shabaab kama walivyokiri. Waliwateka nyara watu ndani ya jingo hilo kwa siku nne.
Pamoja na kupora, vyomo vya habari Kenya vimesema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuwana na wenzao wakati wa operesheni yao kutoka na kile kilichosemekana kuwa ukosefu wa maelekezo mazuri kuoka kwa wakuu wa usalama

 Hii ndio picha iliyoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu wanajeshi wa kenya wakiwa wanatoka na mifuko yenye bidhaa.
Share:

LIST WATAOSHUKA FIESTA 2013(NOUMA SANA)

Hii ndio list ya wasanii watakaodondoka dar uwanja wa leaders club Kinondoni katika show kali ya fiesta mwa huu 2013.Ikionyesha jukwaa kutawaliwa zaidi na miondoko ya azonto baada ya kudondosha wasanii wa 3 wanaofanya staili hiyo maarufu kwa nchi za nigeria na Ghana.Bila kusahau wapenzi wa Reggae wasikose kuja kumuona mwanadada machachari kutoka Jamaika Alaine.

Wasanii wa nyumbani pia hawajaachwa nyuma wapo kibao.

Vilevile mkali wa Dancehall kutoka sweden mtu mzima Mohombi atatondoka na Coconut tree.

NUOMA SAAAAAAAAAAAAANA.

 Huyu ni mwanadada Alaine toka Jamaika anaetamba na ngoma kadhaa za reggae kama vile You are me,Sacrifice n.k na ile ngoma kali NAKUPENDA PIA aliyoshirikishwa na msanii toka kenya Wyre.
\

 Mkali wa miondoka ya dancehall toka sweden Mohombi anayetamba na ngoma kama vile Coconut tree,Bumpy ride n.k


 Mkali anayefukuza nyota ya P Square DAVIDO anaetamba na ngoma kadhaa kama vile Skelewu,Damiduro,Gobe n.k


 Kichwa cha Nigeria mzee wa KUkere Iyanya.


Msanii aliyepata kushirikishwa katika ngoma kadhaa za bongo kama vile kukunja goti ya ay na fa na TUPOGO ya Ommy Dimpoz,na yeye akiwa anatamba na vibao kama vile iva,Touching body,goodtime n.k Jmartins.
Share:

(Angalia)SHOW YA KANYE WEST ILIPOFIKA HAPA IMEZUA MANENO KWA WATU WENGI



Hii ni show ya kanye west inayoitwa Jeezus Tour kilipofika kipande cha kuimba wimbo wake unaoitwa JESUS WALKS alianza kuingia mtu mwenye mavazi meupe akiwa kama Yesu na kuzungumza maneno kadhaa na Kanye west baada ya kutoka huyo jamaa kama Yesu ndio wimbo ukaanza kupigwa na Kanye akaanza Kuperform


HAYA NDIO MAONI MBALI MBALI YA WATU


I just talked to Jesus, he said "what up Yeezus"

So did that stage rise up and down? Because I swear in some of the other videos it looks higher up

Jesus on a triangular stage??? Illuminati alert !!!


this depiction if Jesus is totally wrong, In fact all depictions of Jesus are wrong


Kanye got people worshiping him


yep, went up near the end


There's a difference in believing in some abstract higher power and believing that a man rose from the dead, that eating bread LITERALLY is the flesh of the the Creator of the Cosmos, that of the billions of galaxies in space a guy from Iron Age Palestine was God in the flesh according to conflicting and contradictory sources written centuries after the 'fact'.
I can guarantee 99% of the people in that crowd have never touched a bible, in that sense it's ignorant, but not all are


to call someone ignorant for believing that there's more to life is the most ignorant thing you can do. and how is it self centered? christians believe in a higher power than them



White Jesus made an appearance ha, Kanye knew thats the only way that audience would recognize him
Share:

KAMERA YANASA WANAJESHI WA KENYA WAKIBEBA BITHAA BAADA YA KUOKOA WESTGATE

Picha za wanajeshi wa Kenya waliokwenda katika jumba la Westgate katika juhudi za uokozi na kisha baadaye kuonekena kwenye kamera za CCTV wakiondoka na mifuko ya plasitiki yenye bidhaa za madukani, bila shaka zimewashangaza wengi.
Picha hizo mwanzo zimeonyesha wanajeshi wakiingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamebeba silaha kukabiliana na wanamgambo walioshambulia jengo hilo wiki nne zilizopita na baadaye wakitoka wakiwa wamebeba mifuko hiyo wakiwa na silaha zao kwa wakati mmoja
Hata hivyo haijulikani walichokuwa wamekibeba kwenye mifuko hiyo .
Pamoja na picha za wanajeshi wakiwa wamebeba mifuko, pia kulikuwa na picha zengine zilizoonyesha mashine ya pesa zikiwa zimeporwa ndani ya mikahawa huku picha za alama za risasi kwenye maeneo ya kuhifadhia pesa, pia zikionekana.
Inaarifiwa ilikuwa jaribio ya kufungua hifadhi hizo ambalo halikufanikiwa.
Madai haya ya wanajeshi kufanya uporaji wa maduka katika jingo hilo, yalikanushwa vikali na jeshi la Kenya kiasi cha kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanatoa madai hayo, lakini haijulikani jibu lao litakuwa nini hasa kwa picha hizo za CCTV zilizoonyesha wanajeshi hao wakifanya uporaji.
Wamiliki wa maduka waliorejea kwenye maduka yao bbaada ya shambulizi , walidai kuwa maduka yao yaliporwa ingawa jeshi lilikanusha madai hayo baadhi ya taarifa zikisema kuwa ilikuwa njama ya wafanyabiashara kudai fidia kwa mali zao zilizoharibika.
Sio wanajeshi pekee waliotuhumiwa kwa uporaji, kwani polisi mmoja naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la uporaji baada ya kupatikana na pochi la mtu liliokuwa na damu.
Wangambao wa Al Shabaab waliteka nyara jengo la Westgate kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu 60 pamoja na kuwajeruhi zaidi ya watu miamoja.


Share:

ZITO KABWE ASHANGAZWA NA KATUNI ALIYOCHORWA

Baada ya mapema wiki hii Zito Kabwe kufunguka hadharani kuhusu hesabu za serikali,magazeti kadhaa yamepata kuandika na kuchora katuni mbalimbali kuhusiana na suala hilo.Kupitia account yake ya twitter Zito Kabwe ametweet picha ya katuni moja iliyopo katika gazeti la Tanzania Daima na kuandika maneno yafuatayo.

"Katuni ya Tanzania Daima leo.Inashangaza sana.Siku ya pili leo katuni za suala moja."




Share:

HIVI NDIVYO UFOO SALO ALIVYOJIOKOA

Baada tu ya kupata nafuu Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV na Redio One asimulia baada ya kupata nafuu kutokana na kupigwa risasi hivi karibuni.Ufoo asimulia kama ifuatavyo

“Nyumbani kwetu, pale Kibamba si mbali sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”.

Anasema dada yule alimpa khanga akajifunga na aliposogea barabarani alikutana na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja.

“Nilipoona kuna gari linapita nikainuka kuomba msaada. Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha nikamweleza kwamba nilikuwa nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake anikimbize hadi katika hospitali ya Tumbi na kwamba akifika pale tu aniache mlangoni.

“Si rahisi kuamini, yule mama alikataa kunisaidia akisema alikuwa akiwahi sehemu kumchukua mzazi. Sina la kusema niliamua kumsamehe tu yule mama ingawa niliumia sana,” alisema Ufoo.

Alisema muda mfupi tu baadaye alitokea kijana aliyekuwa na pikipiki, maarufu kwa jina la bodaboda ambaye alimuomba msaada wa kumkimbiza hospitali ya Tumbi na akakubali.

“Yule kijana aliniuliza iwapo nilikuwa ninao uwezo wa kujishikilia vizuri na niliposema nitaweza akanisaidia kupanda katika bodaboda.

“Wakati huo nilikuwa naona kama tumbo linazidi kujaa. Nikiwa kwenye pikipiki kuna wakati nilikuwa nikihisi kwamba naweza nikaishiwa nguvu na kuanguka katika barabara na kisha kupitiwa na gari na kupoteza maisha. Lakini nilipata ujasiri na kujishikilia,” alieleza kwa sauti ya chini
Share:

MANCHESTER UNITED WATOKA SARE,ARSENAL WAPETA

Vinara wa Ligi Kuu ya England, Arsenal wameendelea kujikita hapo baada ya ushindi mnono dhidi ya Norwich.



Wakicheza katika dimba la Emirates, Arsenal walipata mabao yao kupitia kwa viungo Jack Wilshere, Aaron Ramsey na Mesut Ozil aliyefunga mawili.



Norwich walipata bao lao kupitia kwa Jonny Howson, ambapo vijana hao wa Carrow Road walionesha kuwa tishio katika baadhi ya nyakati, lakini Arsenal walifanikiwa kumaliza mechi ya 12 bila kupoteza.



Katika mechi nyingine, mabingwa watetezi, Manchester United waliendelea kudorora baada ya kutoka sare ya 1-1 na Southampton.



Ilikuwa alasiri chungu kwa kocha David Moyes ambaye bado hajaweza kuwaweka vizuri United, ambapo Robin van Persie alifunga bao la kuongoza lakini Saints wakasawazisha dakika moja kabla ya kipenga cha mwisho kupitia kwa nahodha wao, Adam Lalana.



Hali hiyo inawaacha United wakijiuliza iwapo wataweza kutetea ubingwa wao, kwa sababu wamebaki pointi nane nyuma ya vinara wa ligi hiyo.



Manchester City kwa upande mwingine waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham, wakipata mabao yao kupitia kwa Sergio Aguero aliyefunga mawili na David Silva wakati West Ham walifungiwa na Vaz Te.



Huu ulikuwa ushindi wa kwanza kwa City ugenini msimu huu na kuwa furaha kubwa kwa kocha Manuel Pellegrini.


Liverpool waliporeza kasi yao baada ya kwenda sare ya mabao 2-2 na Newcastle, Chelsea wakawafunga Cardiff 4-1 katika mechi ambayo kocha Jose Mourinho alipewa kadi nyekundu kwa utovu wa nidhamu.



Everton walirejea kwenye hali nzuri kwa kuwafunga Hull 2-1, Swansea wakawakung’uta Sunderland 4-0 na Stoke wakaenda suluhu na West Bromwich Albion.



Kwa hali hiyo, Arsenal wanaongoza wakiwa na pointi 19 wakifuatiwa na Chelsea na Liverpool zenye pointi 17 kila moja.



Man City wanafuata kwa pointi zao 16, Southampton wana 15 sawa na Everton, wakifuatiwa na Tottenham Hotspur katika nafasi ya saba huku Man United wakijiburuza kwenye nafasi ya nane.



Sunderland wamebaki mkiani wakiwa na pointi moja baada ya mechi nane, wakati wa pili kutoka chini ni Crystal Palace wenye pointi tatu na Norwich wana pointi saba


Share:

SIMBA , YANGA WATOKA SARE

Simba imeweza kuwabana mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kusawazisha magoli waliyofungwa na kumaliza mchezo wakiwa na sare ya 3-3 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Sare hiyo imezidi kuwafanya mashabiki wa soka waelewe siku zote kwamba mpira ni dakika 90 au mpaka pale filimbi ya mwisho itakapopulizwa na mwamuzi wa kati aliyepewa dhamana ya kuchezesha mechi.

Alikuwa ni Mrisho Ngassa, ambaye alirejea Yanga msimu huu kwa kuanza kuifungia timu yake goli la kwanza katika dakika ya 14 akimalizia pasi fupi ya Hamisi Kiiza ambapo na shuti lake lilisindikizwa wavuni na beki wa Simba, Joseph Owino aliyekuwa kwenye jitihada za kuokoa shambulio hilo bila mafanikio.

Mechi hiyo iliyohudhuriwa na mashabiki zaidi ya 40,000 ilionekana kwamba ni neema kwa Wana-Jangwani pale walipofanikiwa kufunga goli la pili kupitia kwa Mganda Kiiza aliyemalizia mpira uliorushwa na Mbuyu Twite.

Yanga iliendelea kuwanyanyasa watani zao pale walipofunga goli la tatu kupitia kwa aliyeunganisha pasi ya Didier Kavumbagu na kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa magoli 3-0 na mashabiki wao wakiamini siku ya kulipiza kisasi cha 5-0 walichokipata Mei 6 mwaka jana kitatimia.

Hali ilikuwa tofauti kilipoanza kipindi cha pili baada ya King Kibaden, kocha mkuu wa Simba kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kwa kuwaondoa Abdulhalim Homuod na Haroun Chanongo na nafasi zao kuchukuliwa na Said Ndemla na William Lucian ‘Gallas’.

Simba ilianza kucheza kwa kuelewana na safu ya kiungo ambayo ilikufa katika dakika 45 za kwanza ilifufuka na kuanza mashambulizi kuelekea kwenye lango la wapinzani wao.

Betram Mombeki alifanikiwa kuwasimamisha mashabiki wa Simba katika dakika ya 54 kwa kufunga goli la kwanza huko Owino akifunga goli la pili kwa kichwa dakika tatu baadaye na kuwanyamazisha Wana-Yanga ambao hawakuamini kilichokuwa kinaendelea kwenye mchezo huo.

Dakika ya 83, beki mpya wa Simba kutoka Burundi, Gilbert Kaze, aliunganisha kwa kichwa mpira wa faulo uliopigwa na nahodha wake, Nassor Masoud ‘Chollo’ na kuisawazishia timu yake goli la tatu.

Yanga ilionekana kuridhika na matokeo ya kuongoza 3-0 na kuwafanya wachezaji wake wacheze na jukwaa katika kipindi cha pili.

Pia kila mmoja alionekana anataka kufunga na kushindwa kucheza kiufundi kama walivyofanya katika dakika 30 za kwanza za mchezo hali ambayo iliwagharimu na hawataweza kuisahau kwenye kumbukumbu zao.

Simba baada ya kuonekana kuzidiwa mchezo, iliingia kipindi cha pili ikiwa makini kwa kulinda lango lao na vile vile ikifanya mashambulizi kwa kutumia pasi fupi fupi.

Mabadiliko yaliyofanywa yalionekana kuzaa matunda kwa kutengeneza nafasi tano za wazi na tatu kati ya hizo zilizaa magoli.

Kutokana na matokeo hayo bado Azam iliyocheza mechi 10 inaendelea kuongoza ligi sawa na Mbeya City kila mmoja akiwa na pointi 20 na Simba iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 19.

Simba na Yanga yenye pointi 16 iliyo katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi zenyewe zimecheza mechi tisa.

Simba- Abel Dhaira, Nassor Masoud, Haruna Shamte, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhan Singano ‘Messi’, Abdulhalim Homoud/ Said Ndembla, Betram Mombeki/ Zahor Pazi, Amissi Tambwe na Haruon Chanongo/ William Lucian.

Yanga- Ally Mustapha ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/ Simon Msuva.


Share:

"NITAGOMBEA UBUNGE TANGA"-MZEE MAJUTO

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania,Maarufu kama Mzee Majuto amesema anatarajia kugombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM huko mkoni kwake Tanga.Mzee Majuto ameyasema hayo kupitia kipindi cha Amplifaya cha radio clouds FM na Millad Ayo.

TUSUBIRI TUONE UJIO WAKE MZEE MAJUTO KATIKA SIASA.


Share:

Exclusive WIMBO MPYA WA JOSE CHAMILIONE-TUBONGE

Ikiwa na siku kadhaa kutoka kwa wimbo mpya wa Jose Chamilione unaoitwa Tubonge ukiwa katika maadhi ya Gospel.
Kupitia website ya Dj wa Uganda (Dj Erycom) ndiyo ameituma wimbo huu kwa heshima na ushirikiano na mimi Dj Deo kupitia blog yetu ya kitanzania deejaydeo.blogspot.com nauleta kwenu wimbo huo.

Ikiwa katika original version pamoja na Extended version iliyotengenezwa na Dj Deo


isikilize na uidownload hapa









Share:

(Exclusive) HIZI NDIO NYIMBO ZINAZOKUJA KWA KASI

Hii hapa ni wimbo mpya wa Diamond ikiwa ni exclusive akijiuliza siku atakapokufa




Ujio mpya wa Cpwaa ndio huu akiwa na miondoko ya midundo ya kiafro pop isikilize na uidownloada hapa




Maneno aliyotumia katika wimbo huu mimi binafsi ni maneno kuntu ambayo yanahitaji ufikiri kwa makini sana



Humu nakubali zaidi verse ya KABAYSA jamaa kadondoka rymes simple lakini fresh sana.

Share:

KILA IJUMAA NA JUMAMOSI HILI NDILO TUKIO

Kila Ijumaa na Jumamosi sehemu ni moja tu ya kupata BURUDANI nayo ni AMBROSIA BISTRO n BAR iliyopo maeneo ya MBEZI BEACH AFRIKANA ukichukua bajaji  ukimwambia utaletwa mpaka ndani ya mjengo.

Unakaribishwa sana mdau wa burudani


Share:

ANGALIA KUHUSU USIKU WA LEO JUMATANO

New palm view bar na CLUB LITE maeneo ya kigogo wanakuletea bonge la burudani.Upande wa nje wa BAR kutakuwa na wakali wa mauno kundi zima la BAIKOKO wakiwa wanatoa burudani kabambe bila kiingilio.

Baada ya hapo sasa burudani inahamia ndani ya mjengo yaani CLUB LITE eneo hilo hilo ukiwa na wakali wa kukimbiza disko jijini yaani YOUNG DJs hapo utamkuta Dj Valela na Dj Deo.

Kiingilio ni kidogo tu sh 3000/= tu unazama ndani ukutane na watoto wakali.

Usikose !!!!!!


Share: