NE YO NDIO MSANII ATAKAEPIGA SHOW KWENYE MTV MAMAZ-2015

Tuzo kubwa za muziki Africa zijulikanzazo kama MTV MAMA2015 zitakzofanyika tarehe 18 july 2015 huko KWAZULU NATAL - SOUTH AFRIKA zitapambwa na msanii wa kimataifa kutoka marekani NE YO.

Katika tuzo hizo ambazo zimeweza kuwataja wasanii wawili wa TANZANIA kuwania vipengere kadhaa vikiwemo MSANII BORA WA KIUME(BEST MALE) , WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA(BEST COLLABO) na MTUMBUIZAJI BORA(BEST LIVE) akiwa amekaa Msanii DIAMOND katika vipengere hivyo.

Vilevile katika kipengere cha MSANII BORA WA KIKE(BEST FEMALE) akiwa amekaa VANESA MDEE akishindana na wasanii wengine kutoka afrika.

Ili kuweza kuwapigia kura wasanii hao wa tanzania unaweza kuingia katika link ifuatayo

VOTE FOR MTV MAMA2015



Share:

DIAMOND NA VANNESA MDEE WATAMBA TRACE TV

Kituo kikubwa kabisa cha televisheni cha trace kinachorusha NYimbo 10 bora za Afrika,kwa sasa Watanzania washika kasi baada ya chat hizo kushikwa na wasanii wawili toka Tanzania

Nafasi ya 8 imekamatwa na VANNESA MDEE FT. K.O -NOBODY BUT ME

Nafasi ya 2 imekamatwa na DIAMOND FT. MR.FLAVOUR- NANA



Share:

MADJ KENYA WAGOMA KULIPIA WANAPOPIGA NYIMBO ZA KIKENYA

Skendo hii imeanzia hivi karibuni kufuatia kuzaga kwa taarifa kuwa wasanii wa kenya wanadai kulipwa pindi nyimbo zao zinapochezwa na madj nchini humo.Hali ambayo imeleta mtafaruku mkubwa kati ya madj wa kenya na wasanii na kuna fununu ya kuwa baadhi ya madj wa kenya wamefuta kabisa nyimbo za wasanii wa kenya katika vifaa vyo vya kuhifadhia nyimbo zao.
Hata kufikia madj wengine mfano wa redio kuacha kabisa kucheza nyimbo za wasanii wa kenya na badala yake wanacheza nyimbo za mataifa mengine kama vile Tanzania,Nigeria,Uganda n.k

Hali imekkuwa tete zaidi kufuatia maoni mbalimbali kutoka katika kikundi kubwa la madj ambalo lipo katika mtandao wa facebook.

Hizi ni baadhi ya post za hivi karibuni kufuatia sakata hilo huko nchini kenya......



Deejay Shock
June 21 at 3:18am
I am wondering if artistes are aware of how serious the licence issue is to their own livelihood. Several Djs have deleted their whole Kenyan music collections, some are issuing disclaimers that they will no longer accept music submissions from Kenyan artistes, the hashtag going round now seems to be ‪#‎RIPKenyanMusic‬.
If the artistes understood what was happening, wouldn't they speak to these collecting bodies about the effect they are having on the artiste by harrassing Djs?



Vinnie DjKrypt
Yesterday at 4:46am
‪#‎KenyanArtists‬.......Are you serious?......you walk into my booth with ya cd in ya hands, give it and plead with me to help you push for it so that people can listen to it, you later turn against me and wants me too to pay you for marketing ya music in the name of collecting royalties......How much royalty did you pay me to push it for you.......‪#‎asanteyapunda‬ ni mateke......‪#‎RIPKenyanMusic‬


Steve Karimi
June 21 at 4:07am
my fellow deejayz kindly give me advice on what to do with kenyan music coz clearly i dont want trouble.



BOFYA HAPA UINGIE GROUP LA FACEBOOK KUSOMA ZAIDI

Share:

ALI KIBA ANG'ARA KATIKA TUZO ZA MUZIKI KILL MUSIC AWARDS

Usiku huu kile kinyang'anyiro cha ugawaji wa tuzo za muziki nchini kijulikanaco ka kill muzik awards kimehitimishwa kwa wasanii mbalimbali na makundi mbali mbali ya muziki kupata tuzo hizo.
Lakini kubwa zaidi ambalo limezua gumzo nchini kuwaangalia zaidi wasanii wakubwa wawili wa muziki nchini yaani DIAMOND na ALI KIBA.
Wengi wetu tunajua kuwa kuna ubishani mkubwa sana kati ya wasanii hao wawili mpaka kufikia watanzania wenyew kutengeneza makundi kati yao yaani utakuta kuna TEAM KIBA na TEAM DIAMOND ambapo usiku huu amejidhihilisha mbabe nani katika kuwania tuzo hizo.
Mkoani MTWARA katika baa moja kubwa  inaitwa FIRE CANTEEN hali ilikuwa tete baada ya TEAM hizo mbili kutambiana pindi tu kipenga cha tuzo hizo kilipoanza.
Hali ilianza kutia faraja baada ya DIAMOND kuonyesha matumaini yake mwanzoni katika kipengele cha WIMBO BORA WA MWAKA WA ZOUK RUMBA mbapo wimbo wa NTAMPATA WAPI uliweza kunyakua tuzo hiyo.
Pia katika kipengere kingine cha VIDEO BORA YA MWAKA kupitia wimbo wa MDOGO MDOGO ulimpa tuzo pili DIAMOND.
Hali ikabadilika baada ya ALI KIBA kuanza kushika kasi na kuchukua tuzo 5 katika vipengere hivi....
1.WIMBO BORA WA MWAKA
2.MWIMBAJI BORA WA KIUME(Bongofleva)
3.MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME
4.WIMBO BORA WA AFRO POP na
5MTUNZI BORA WA MWAKA

Kupitia ACCOUNT yake ya INSTAGRAM, Ali kiba Amepost video akiwashukuru wote waliomwezesha kupata tuzo hizo.Kwa sasa ALI KIBA yuko UK katika kazi yake na muziki ndio maana hakuonekana ukumbini wakati wa utoaji wa tuzo hizo.




Share:

HAWA NDIO WALIOSHINDA TUZO ZA KILL MUSIC AWARDS(KTMA 2015)

Ushindani ulikuwa mkubwa sana katika vipengere vyote vilivyowaniwa na wasanii hata makundi mbalimbali ya muziki tanzania na afrika mashariki.
Watanzania wengi walikuwa na shauku ya kujua mkali nani kati ya ALI KIBA na DIAMOND lakini ubisi umekwisha kufuatia kupatikana kwa tuzo hizo kati ya wasanii hao wawili.
Ili kujua nani kamuongoza mwenzake angalia washindi wa tuzo hizo katika list mbalimbali hapa chini.

1. KUNDI BORA LA MUZIKI (BONGO FLEVA)   - YA MOTO BAND

2.KUNDI BORA LA MUZIKI (TAARABU)            - JAHAZI MORDEN TAARAB

3.MWIMBAJI BORA WA KIUME (BENDI)           - JOSE MARA

4.MWIMBAJI BORA WA KIKE(TAARABU)         - ISHA MASHAUZI

5.WIMBO BORA WA MWAKA(BONGO FLEVA) -MWANA(Alikiba)

6.WIMBO BORA WA KISWAHILI (BENDI)        - WALE WALE(Fm Academia)

7.MWIMBAJI BORA WA KIUME (TAARABU)    -MZEE YUSUPH

8.WIMBO BORA WA RNB                                     -SISIKII(Jux)

9.MWIMBAJI BORA WA KIKE (BONGO FLEVA)  -VANESSA MDEE

10. MWIMBAJI BORA WA KIUME (BONGO FLEVA) -ALI KIBA

11.MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE                         -VANESSA MDEE

12.MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME                    -ALI KIBA

13. WIMBO BORA WA HIP HOP                            - KIPI SIJASIKIA(PROF JAY)

14.WIMBO BORA WA REGGAE/DANCEHALL - LET THEM KNOW(Maua)

15.RAPA BORA WA MWAKA (BENDI)               -FEGASON

16.MSANII BORA WA HIP HOP                           -JOH MAKINI

17.WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI     -SURA YAKO (Sauti Sol)

18. MTUNZI BORA WA MWAKA (TAARABU)    -MZEE YUSUPH

19.MTUNZI BORA WA MWAKA (BENDI)            -JOSE MARA

20.MTUNZI BORA WA MWAKA (HIP HOP)        -JOH MAKINI

21.MTAYARISHAJI(PRODUCER) BORA WA NYIMBO(BONGO FLEVA) -NAH REAL

22. MTAYARISHAJI(PRODUCER) BORA WA NYIMBO(TAARABU)      -ENRICO

23. MTAYARISHAJI(PRODUCER) BORA WA NYIMBO (BENDI)           -AMOROS


24- VIDEO BORA YA MWAKA                     -MDOGO MDOGO(DIAMOND)

25.WIMBO BORA WA AFRO POP                -MWANA(AliKiba)

26.WIMBO BORA WA ZOUK RUMBA         -NTAMPATA WAPI(Diamond)

27.WIMBO WENYE ASILI YA KITANZANIA   -WAITE(Mrisho Mpoto)

28.MSANII BORA CHIPUKIZI           -BARAKA DA PRINCE

29.WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA     -KIBOKO YANGU(Mwana FA feat Ali Kiba)


30.BENDI BORA YA MWAKA                    -FM ACADEMIA

31.MTUNZI BORA WA MWAKA               -ALI KIBA


Share:

COLLABO NYINGINE AFRIKA NA MAREKANI NI HII HAPA

Baada ya Davido kupaa mpaka Marekani na kufanya ngoma na mkali wa rap Meek Mill,msanii mwingine wa Afrika kutokea pande za Ghana anaitwa Sackodie nae amepaa mpaka marekani na kufanya ngoma na mkali mwingine wa rap huko anaitwa ICE HOOD.




Share:

VIDEO YA 'FANZ MI' YA DAVIDO & MEEK MILL YAONGOZA KUTAZAMWA NDANI SAA 24

Kupitia mtandao mmoja umeripoti ya kuwa haijawahi kutokea kwa msanii wa nigeria kufanya video na ikapata kutazamwa mara nyingi zaidi ndani ya saa 24.
Rekodi hii imeonyeshwa na davido kupitia video yake mpya aliyoiachia hivi karibuni akiwa na rapa wa kimarekani wa kuitwa Meek MILL.
Mtandao huo umeripoti na kusema kuwa video hiyo ya wimbo unaokwenda kwa jina la FANS MI ilipata kutazamwa ma Mil.2 na zaidi ndani ya saa 24.



Share:

PICHA HII YA MILEY CYRUS YAZUA MGOGORO

Msanii wa muziki kutoka Marekani mwanadada MILEY CYRUS usiku wa kuamkia leo amepost picha akiwa uchi wa mnyama kupitia acount yake ya facebook.Baadhi ya washabiki wake wamjia huu kwa maneno makali na wengine kuamua kusema kuwa hana wazazi.
Hii si ngeni kwa mwanadada huyu kupiga picha za uchi na ameonekana mara kadhaa akiwa uchi wa mnyama hata katika video ya wimbo wake wa WRENKING BALL.

BOFYA HAPA KUTAZAMA MOJA KWA MOJA PICHA HIYO KUPITIA FACEBOOK
MILEY CYRUS PICHA YA UCHI

Share: