Mbowe alisema kutokana na tukio hilo ambalo limeua watu zaidi ya watatu, CHADEMA imeamua kulifanya ni la kitaifa na wabunge wake watashiriki kwenye maombolezo.
Alisema kuanzia leo wabunge wote wa CHADEMA hawatahudhuria vikao vya Bunge na watajumuika mkoani Arusha hadi misiba yote itakapomalizika.
Alisema wanatarajia kufunga mahema katika eneo la tukio na marehemu wote wataagwa katika eneo hilo ambapo ibada zote za Kiislamu na Kikristu zitafanyikia hapo