KIFO CHA MICHAEL JACKSON-"ALIKUFA KWA KUKOSA USINGIZI"

Conrad Murray alikuwa akimpa dawa za kutuliza maumivu kwa miezi miwili mfululizo kila siku hali iliyopelekea mwili kuchoka kila wakati. Inaelezwa kuwa, dawa hizo zina kawaida ya kumnyima mtu usingizi na zinaweza kumfanya kupoteza fahamu. Daktari bingwa na mtaalamu wa magonjwa kichwa, Charles Czeisler amesema Jackson aliyefariki akiwa na miaka 50, huenda alikufa aidha, kwa sababu ya kukosa usingizi muda mrefu, au kutumia kwa muda mrefu dawa za kutuliza maumivu alizokuwa akipewa na Murray. Siku chache kabla ya kifo chake, ilielezwa kuwa Jackson hakuweza kucheza japo kidogo au hata kukumbuka baadhi ya maneno kwenye nyimbo zake.

Dr Czeisler amebainisha kuwa, dalili za tatizo lililomuua liliendelea muda mrefu kwa sababu ya matumizi ya dawa hizo, lakini zaidi ni kukosa usingizi hali iliyofanya mwili kuchoka kila wakati na hivyo kuathiri utendaji wa kawaida wa mwili.

“Katika hali kama hii, sehemu nyingi za mwili haziwezi kufanya kazi kwa usahihi. Ili mwili wote ufanye kazi vizuri, kila kiungo kinahitaji kuwa kwenye hali nzuri,” alieleza daktari huyo bingwa.

Familia ya Jackson inaishitaki taasisi ya kuandaa matamasha ya AEG iliyomuajiri Murray kama daktari.

Los Angeles, Marekani. Michael Jackson huenda akawa binadamu wa kwanza kukosa usingizi kamili kwa siku 60, wataalam wamebaini. Daktari wake binafsi wa Jackson.

Michael Jackson

source mwananchi
Share: