MAPOKEZI YA DAVID BECKHAM YAUMIZA WATU CHINA


Watu 7 wanaelezewa kuumia vibaya baada ya kutokea fujo kwa mashabiki waliokuwa wanataka kumwona mchezaji nyota David Beckham huko China.

Kati ya watu hao walioumia kwa ajari hiyo ni polisi watatu,walinzi wawili na wanafunzi wawili.

Ziara hiyo ya nyota huyo wa mpira wa miguu nnchini china ikiwa ni kutembelea chuo cha mpira wa miguu nchini humo.

Habari zinasema kuwa pindi tu nyota huyo alipofika katika uwanja wa mpira mmoja,mashabiki wapatao zaidi ya 1000 waliokuwa hapo walikuwa na shauku ya kutaka kumuona hiyo walianza kupalamia geti na kuvuruga mistari iliyopangwa na polisi na walinzi katika uwanja huo mpaka kufiki kutokea kwa majeruhi hao.






Share: