MABOMBA YA KUSAFIRISHA GESI YAWASILI DAR


Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda amepokea shena ya kwanza ya mabomba kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mtwara na Songo songo hadi Dar es Salaam huku akiwataka wanachi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha mradi huo ambao una tija kubwa kwa uchumi wa taifa. Mh Pinda amepokea shehena hiyo  katika bandari ya Dar es Salaam ambapo amesema inashangaza kuona baadhi ya watu kwa makusudi kabisa wanapotosha ukweli wa mambo kuhusu mradi huo.

 
Awali wakizungumza kuhusu mradi huo waziri wa  nishati na madini Mh profesa Sospeter Muhongo amesema sasa  serikali imeanza safari ya maendeleo wakati mkurugenzi mtendaji wa shirika la maendeleo ya petrol nchini TPDC Bw  Yona Kilagane amesema hiyo ni awamu ya kwanza ila zinakuja jumla ya meli 12 zenye shehena hiyo.
 
Kwa upande wa balozi wa China hapa nchini  Dk Lu Youging  ambao ndio wajenzi wa mradi huo wamesema  wataendeleza mahusiano mema ambao yamekuwepo kati ya China na Tanzania kwa muda mrefu huku akitolea mfano ujenzi wa reli ya Tazara.
Share: