BINGWA WA NGUMI(MASUMBWI) AFARIKI DUNIA


Bingwa wa zamani wa dunia katika ndondi uzani wa Heavyweight mmarekani Ken Norton amefariki akiwa na umri wa miaka 70
Anakumbukwa zaidi kuwa kumshinda gwiji wa masumbwi Mohammad Ali mwaka 1973.
Sawa na mabondia wengi wa uzani mkubwa enzi zake, Ken Norton anakumbukwa kwa jinsi alivyopigana na Mohamed Ali.
Na kwenye pigano lao la kwanza la mwaka 1973, Norton ambaye hadi wakati huo hakujulikana sana alimkomesha Ali na kumshinikiza makonde tangu mwanzo hadi mwisho.
Norton alivunja taya la Ali kwenye pigano la raundi 12, akawa bondia wa pili kumshinda Mohamed Ali tangu alipoanza ndondi za kulipwa.
Katika mapigano yaliyofuatia, baadaye mwaka huo wa 73, Ali alilipiza na kumshinda Norton, na TENA mara nyingine miaka mitatu baadaye kwenye pigano lao la mwisho katika uwanja wa Yankees, mjini New York. Lakini hata hivyo Norton baadaye alitwaa taji la ulimwengu la WBC, kabla ya kulipoteza kwa Larry Holmes mwaka 1978.
Norton, bingwa wa Marekani uzani wa Heavyweith alikuwa ameanza mchezo wa ndoni mwaka wa 63 akiwa katika jeshi la wanamaji. Lisilosahaulika daima ni pigano hilo la mwaka 73 alipomshinda kumshinda Mohammed Ali, akimvunja taya. Alistaafu masumbwi mwaka wa 81.
Alishiriki mapigano 50 ya ndondi za kulipwa, na afya yake ikadorora ingawa alikataa kuulaumu mchezo wa masumbwi kama sababu ya maradhi yake. Alitatizwa na ugonjwa wa kiharusi mara kadhaa. Afya yake imemsumbua kwa mda hadi kufariki kwake akiwa mwenye umri mdogo wa miaka 70



Share: