Baadaye kila panya hufanya mafunzo kwenye eneo ambalo kuna mabomu ya ardhini yaliyofukiwa na vifaa ambayo huzuia mlipuko. Ikiwa panya ameweza kunusa na kutambua yalipo madini asilia ya TNT huwa anasimama na kuanza kufukua sehemu hiyo ya ardhi iliyofukiwa bomu. Kuwafundisha panya kunachukua muda wa mwaka na inagharimu dola za Kimarekani $6,000 sawa na Euro 4,670
Wakati wa mafunzo panya hupewa zawadi kwa kufuzu vizuri kwa sauti maalumu ambayo inaashiria kufuzu kwake na kupewa kipande cha ndizi kama zawadi. Panya aliyefuzu vizuri huwa ana uwezo wa kuzunguka mita 400 za mraba kwa siku, wakati eneo kama hili litamchukua binadamu wiki mbili ili kuweza kugundua wapi kumefukiwa bomu
Kulinganishwa na mbwa, panya wanaweza kutumiwa na mtu yeyote kwani hawana tabia ya kutokuwa na mahusiano ya karibu na mtu aliyemfundisha kama walivyo mbwa. Panya anaweza kufanya kazi ya kufichua mabomu, hata kama aliyemfundisha hayupo na huwa wanafanya kazi vizuri kwa ufanisi na mtu yeyote. Hakuna shida kwa panya aliyefundishwa Tanzania, kwenda kufanya kazi Msumbiji, Angola,Thailand na Kambodia
Hadi kufukia sasa nchini Msumbiji, zaidi ya mita za mraba milioni 6,5 za ardhi zimeshachunguzwa na mabomu 2,000 yaliyotegwa ardhini yamepatikana na kuharibiwa, pia bado mabomu 1,000 kuteguliwa na bunduki na silaha nyingine ndogo 12,000 zilipatikana. Na mpaka sasa kuna makundi saba yenye watu 54 ambayo yanashughulika na kazi ya kutegua mabomu kwa kuwatumia panya