Mchana wa leo eneo la West gate kumeonekana moshi mzito ukiwa unavuka kutokea ndani ya jengo lililoshambuliwa jana na kikundi cha kigaidi cha Al shabaab nchini kenya.Kwa mujibu wa BBC wanasema wanajeshi wa Kenya walilipua mabomu ili kuendelea kukabiliana na tukio hilo.Pia mpaka sasa inasemekana watu waliofariki yafikia 69 na na wengine mamia wamejeruhiwa huku idadi isiyojulikana wakiwa wameshikiliwa mateka na Al Shabaab!!