MFUMO WA DIGITAL KUINGIA MIKOANI

TAARIFA KWA UMMA


RATIBA YA UZIMAJI  WA MITAMBO YA UTANGAZAJI YA ANALOJIA AWAMU YA PILI

Ndugu wananchi, napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa Awamu ya Pili ya Uzimaji wa Mitambo ya Utangazaji ya Analojia itaanza rasmi mwezi Machi mwaka huu. Awamu hii ya Uzimaji inaanza baada ya Serikali kujiridhisha na matokeo ya tathmini ya uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya analojia awamu ya kwanza kwenye miji saba ya Dar Es salaam, Tanga, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Moshi na Arusha. Tathmini hiyo imeonyesha kuwa asilimia 89% ya watanzania kwenye miji hiyo wamehamia kwenye mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali. 

Ninaamini kuwa asilimia kumi na moja ya watanzania waliobaki kwenye miji hiyo watakuwa wameingia katika mfumo wa dijitali hadi hivi sasa.

Ndugu wananchi, Awamu ya Pili ya Uzimaji wa Mitambo ya Utangazaji ya Analojia itaanza mwezi Machi mwaka huu katika miji tisa na kukamilika mwezi Oktoba 2014. Miji hiyo ni Singida, Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma, Morogoro, Kahama, Iringa na Songea. 


Natoa wito kwa wadau na wananchi wote kushirikiana na Serikali katika kutekeleza vema zoezi hili la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya analojia kwa manufaa ya Taifa letu na wananchi wote kwa ujumla.

Asanteni sana.

Imetolewa na:
Prof. Makame M. Mbarawa (MB.)
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
DAR ES SALAAM
21/02/2014
Share: