Baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa kuanzia mwishoni mwa mwaka jana hivi sasa huu (katika picha) ndio muonekano mpya wa deca inn kwa wale wanaoishi njia ya kuelekea bagamoyo watakuwa wanapajua.Kiukweli kwa sasa muonekano wake una hadhi ya juu sana,ambayo kila mtu akihitaji kupaona au kufika eneo hilo ataweza kurefresh mind yake na kuenjoy.Pia kwa kuona umuhimu wa watoto kupenda michezo mbali mbali hasa bembea,kuna sehemu imewekwa bembea kwa ajili hiyo.
Hivyo unaweza kufika na famili yako bila kupata usumbufu wowote ule na kutuliza akili yako.
Kwa hakika hakuna buguza ya makelele wala ualifu wa aina yoyote.
Hata mimi mwandishi wa habari hii napenda kukuambia kuwa tembelea siku moja utaweza kuona ukweli wa ninachokuambia.Mazingira mazuri,upepo mwanana,chakula na vinywaji mbalimbali,bila kusahau kuna hoteli kwa ajili ya mapumziko mbali mbali iwe honeymoon n.k
Vile vile kwa wale wapenzi wa burudani kila siku ya ijumaa na jumamosi kuna muziki maalum wa kisasa na wa enzi zileee....mida ya usiku kuanzia saa 2...
Jaribu kufika siku moja na utaamini maneno yangu.
ANGALIA HIZI PICHA ZA MCHANA NA JINSI ILIVYO USIKU