Kuna
taarifa za kikundi cha magaidi wa Al-Shabab kuvamia kituo cha polisi
katika mji mdogo wa Mandera uliopo mpakani mwa Kenya na Somalia.
Shambulizi hilo ambalo limefanyika mapema leo limesababisha vifo vya
polisi wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa, huku magaidi hao wakichoma
moto magari 11.
Duru za kiuchunguzi zinaonesha kwamba hiyo ni
sehemu ya mfululizo wa mashambulizi yaliyoandaliwa na Al-Shabab baada ya
lile la Westgate, jijini Nairobi.