Kutoka kwenye ukurasa wake wa facebook na twitter Mrembo huyo aliandika maelezo yafuatayo
KATIKA FACE BOOK
“Jumamosi iliyopita nilikuwa kwetu songea vijijini kama mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michezo ya Umisseta ngazi ya wilaya. Lakini vile vile nilipata nafasi kutambulisha program ya #KidotiTime itakatoingizwa kwenye ratiba za shule takribani 27 kwa kuanzia. Program hii ni kusaidia wanafunzi kujitahidi darasani huku wakigundua na kuendeleza vipaji vyao vingine. Sengwile”
KATIKA TWITTER
“Naanzisha kitu kinaitwa #KidotiTime kwenye shule 27 huku songea vijijini. Nashukuru walimu woooote kulipokea hili kwa moyo mmoja”
“#KidotiTime imeanza vijiji kutoa hamasa kwa watu wote kuwa hata huku kuna vipaji na vinafaa viendelezwe”
“#KidotiTime ni njia tu mmoja wapo ya kuvutia wanafunzi pia kufanya vizuri shuleni. Unaweza kuwa mwimbaji mzuri na kufanya vizuri darasani.”