WATU 91 WADAKWA GHASIA ZA GESI

Katika hotuba waziri Nchimbi alisema kuwa watu 91 ndio wanashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na vurugu zilizotikea mtwara mapema wiki hii.Vilevile waziri Nchimbi aliongeza kwa kusema kuwa serikali imeapa kuwa damu za askari 4 zilizomwagika kutokana na ajali ya gari la jeshi iliyotokea Nachingwea wakati wanaenda Mtwara kudhibiti vurugu hizo haitamwagika bure.
Aliendelea kwa kutaja pia athari zilizojitokeza kutkana na vurugu hizo kuwa ni pamoja na
1.kuchomwa moto mahakama ya mwanzo iliyopo mitengo
2.kuchomwa moto kwa nyumba ya mwandishi wa habari wa tbc
3.kuvunjwa na kuibiwa katika nyumba ya askari wanne
4.kuibiwa vitu mbalimbali katika ofisi ya kata

MH. Nchimbi alitaja kuwa mtu aliyefariki dunia ni Karim Shaibu pamoja na askari wawili walijeruhiwa kutokana na bomu la kishindo.

Waziri huyo pia akitoa kauli kuhusu askari waliokufa ajalini alisema "Askari hawa wamekufa na kujeruhiwa wakiwa kazini kutekeleza wajibu wa kuwalinda watanzania,damu zao hazitamwagika bure.Mungu aziweke pema roho za marehemu na awape nafuu majeruhi"


Share: