HALI YA MANDELA YABADILIKA GHAFLA"CRITICAL CONDITION"

Hali ya raisi wa zamani wa Afrika Kusini.Nelson Mandela imebadilika ghafla jioni ya leo na kuwa mbaya katika muda wa saa 24 zilizopita.
Raisi wa nchi hiyo Jacob Zuma na makamu wa raisi ANC Cyril Ramaphosa walipata fursa ya kumtembelea Mandela hospitalini jioni hii.

Mh.Zuma alitoa tamko kuhusiana na hali hiyo "Madaktari wanafanya kila linalowezekana kufanya ili hali yake  iweze kuwa salama"Zuma aliendelea kusema "yupo kwenye mikono salama"

Mh.Mandela amekuwa akisumbuliwa mara kwa mara kwa miezi hii ya karibuni na mpaka sasa yafikia mara 4 amekimbizwa hospitali tangu mwezi wa 12.

Mr Zuma amerudia tena kuiomba Afrika Kusini na dunia kwa ujumla kumwombea Mandela arejee kwenye hali ya kawaida.

Katika kelezea zaidi hali inayoendelea hivi sasa Mr Zuma alisema"Kuna madaktari 7 ambao wapo kufuatilia hali yake muda wote".

 Watoto wakituma salamu za pole kwa Mandela


Nelson Mandela

Popular posts from this blog