Hatimaye ile ndoa iliyokuwa ikusubiriwa kwa hamu kubwa na ndugu jamaa na marafiki wa mkongwe wa filamu Tanzania Suzan Lewis maarufu kama Natasha imewadia baada ya juzi kufanyiwa sherehe ya “kufundwa” kabla ya kukabidhiwa kwa mumewe hivi karibuni.
Katika habari iliyoripotiwa kwa picha na mtandao wa global publishers sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Tandika Maghorofani, Dar ambapo iliandaliwa na rafiki wa karibu wa Natasha aliyejulikana kwa jina moja tu la Nuru.
Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mastaa wengi mavazi yalionekana kuwa ya kiasili zadi na kina dada hao kuonekana wakikata viuno vya nguvu kumpongeza Natasha
Baada ya yote hayo kukamilika, msafara wa kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo ulianza huku ngoma zikiendelea kupigwa mpaka nyumbani kwa Natasha
Akizungumzia shughuli hiyo, Natasha alisema: “Nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu. Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia.”