WEMA & KAJALA PETE NA KIDOLE

Baada ya siku chache za magazeti ya udaku nchini kuripoti kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa karibu sana kati ya mwanadada Wema sepetu na Muigizaji mwenzake Kajala masanja, tuliamua kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa suala hili ili tusije kuipotosha jamii kwa habari za zisizo na ushahidi wowote.

Katika habari iliyoripotiwa na blogs na magazeti kadhaa ya udaku kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema kuwa chanzo ni vitendo vya mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala kwenye dili anzopata za kucheza filamu na hasahasa kumkosesha dili ya kwenda china kufanya filamu aliyoalikwa na watanzania waishio nchini humo.Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta hewani wasanii hawa ili tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada Kajala alikuwa wa kwanza kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo na kuwashangaa wanaoziandika wanazipata wapi.

“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala

Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema

“Wolper nimekutana naye kwenye party ndo tukaamua kupiga picha, au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu mwingine zaidi ya wema? Wolper ni rafiki yangu” Alisisitiza Kajala

 Tulipojaribu kumtafuta wema simu yake ilikuwa haipokelewi na baadaye ilipokelewa na alisema yuko location anatengeneza filamu na mwigizaji Rado hivyo tumtafute baadaye

Popular posts from this blog