RATIBA YA OBAMA LEO

Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Obama ambaye atafuatana na Mkewe Mama Michelle atapokelewa na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Baada ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete. Aidha, atafanya mkutano na Wafanyabiashara na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.

Tarehe 2 Julai 2013, Mhe. Rais Obama atatembelea Mitambo ya kufua Umeme ya Symbion iliyopo Ubungo, Dar es Salaam na kuzindua rasmi Mpango Maalum wa Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na Marekani (Power Africa Initiative).

Mpango huo utaanza na nchi saba ambazo ni: - Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Sudan Kusini.

Mh.Barrack Obama anatarajiwa kuondoka nchini julai 2.

Share: