B-FRIENDS-KUNDI LA BONGO FLAVA LINALOKUJA KWA KASI

Kundi la muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva,B-FRIENDS linaundwa na vijana KISU na OZB lenye maskani yake hapa jiji dar es salaam limesema kuwa limedhamilia kuteka soko  la muziki nchini na nje ya nchi pia.Kundi hilo ambalo mpaka sasa limefanya ngoma kadhaa ambazo zimepata kutamba zaidi katiika mitandao mbalimbali duniani,vile vile kundi hilo limeweza kutengeneza remix ya wimbo wa BUSY SIGNAL-COME OVER(MISSING YOU. Ukiwa kwa lugha ya kiswahili na kuupa jina ukiitwa WE NI WANGU.Wimbo huo umeweza kutamba katika mtandao wa you tube pindi tu uliipoka video yake.....

HII HAPA AUDIO YA WIMBO HUO ULIOTUMIA BEAT YA BUSY SIGNAL...HII HAPA NI CLUB VERSION.....DOWNLOAD NA USIKILIZE HAPA





Baada ya hapo wakaja kutoa kibao kilichokwenda kwa jina la GALASA wakiwa wamemshirikisha ALLY KIBA.Isikilize hapa pia





Wakazidi kupiga hatua kwa kutoa kibao kingine chenye beat ya kwaito ya Dj cleo.Wimbo huo unaweza kuuangalia you tube unaitwa AZOGO.

Kuonyesha wao ni wakali wametoa kibao kipya kabisa ambacho kwa sasa leo nakitambulisha rasmi kwako mpenzi na msomaji wa blog hii.Unaombwa sapoti yako ili kuweza kufikisha malengo yao vijana hawa ambao wameonyesha juhudi katika muziki wakizazi kipya.
Wimbo huu mpya unaitwa NAKU LOVE ameshirikishw mwnadada anaitwa ASHILIY kutoka UGANDA......USIKILIZE HAPA CHINI UKIWA KATIKA ORIGINAL VERSION na EXTENDED VERSION ambayo imetengenezwa na Dj Deo kuonyesha kwamba beat ya wimbo huu ni kali sana.







Changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa vijana hawa wamesema wanahitaji mtu wa kuwasapoti na kuwapa promo ya kutosha ili waweze kufikia malengo yao.Ewe mdau wa muziki unaependa kuendeleza vipaji vya vijana hawa jitokeze leo kuwapa sapoti na kuwapromoti zaidi.

Share: