MTWARA BADO HALI TETE

Habari zilizonifikia hivi leo mpaka muda naingia kupost habari hii ni kuwa leo asubuhi eneo la maduka na soko lililopo Magomeni mkoani mtwara,maduka kadhaa na nyumba za baadhi ya wananchi zimechomwa moto.
Pia mwanafunzi mmoja wa chuo amefikishwa hospitali ya mkoa huo baada ya kujeruhiwa vibaya na risasi katika eneo la mguu wake.
Vilevile mwanamke mmoja inasemekana alikuwa mjamzito amefariki dunia.
Kwa upande mwingine huduma mbalimbali za kijamii zimesimama,na usafiri wa kuingia mtwara hasa eneo la magomeni umekuwa mgumu kwa kile kinachoelezewa kuwa ni hofu ya fujo hizo

HILI NI ENEO LA SOKO NA BAADHI YA MITAA IKIWA KIMYA BADO




Share: