Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amesema kuwa
amefahamishwa na madaktari wanaomtibu kuwa, hali
ya Mzee Mandela ambaye
anaendelea kupokea
matibabu katika hospitali
moja mjini Pretoria imeimarika.Siku ya Jumanne rais Zuma, alisema
kuwa nchi yote inazidi kumwombea Mzee Nelson
Mandela ili apate afueni haraka.Rais Zuma
amesema amefurahishwa na jinsi hali ya rais huyo
inavyoendelea kuimarika, baada ya kudhohofika sana siku chache zilizopita.
Rais huyo wa zamani amelazwa hospitalini
Pretoria, ambako anatibiwa maambukizi ya mapafu.
Katika taarifa yake rais Zuma amesema japokuwa
Mandela ameathirika sana, madaktari
wanaomshughulikia wanafanya kazi nzuri.
Rais huyo mstaafu wa Afrika Kusini, amelazwa
hospitalini kwa siku ya tano leo ambako
anapokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu