Makala-KUKOSA MAFANIKIO KIMAISHA

Imeandikwa na Mtabiri Maalim Hassan


KUKOSA MAFANIKIO KIMAISHA:

Je umejiuliza kwa nini hupati mafanikio kimaisha, mambo yako yanakwama na unakosa unachokitaka. Unajaribu kila njia kupata mafanikio lakini inashindikana?

Mojawapo ya mambo yanayokuangusha kimaisha ni Tabia yako, ukifikiria unaweza kufanya jambo utafanya, na ukifikiria kwamba huwezi kufanya hutoweza, je ni kwa nini?

Jibu hilo linapatikana katika nyota na maelezo yake ni kama ifuatavyo:

WATU WA NAMBA 1:

Ukiwa umezaliwa tarehe 1, 10, 19 au tarehe 28 au jina lako likianzia na A J S, tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana na tabia ya Unyonge na kutegemea sana watu achana nayo.

Pili acha kujivuna, acha kuringa na usipende kuwa kimbele mbele katika mazungumzo, Tabia hiyo inawafanya watu wakukimbie.

Tatu tabia yako ya kutokuwa na subira, kulazimnisha mambo na kujisifu haikusaidii achana nayo kabisa.

WATU WA NAMBA 2:

Ukiwa umezaliwa tarehe 2, 11, 20 au tarehe 29 au jina lako likianzia na B K na T, tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana na wewe kuwa na aibu sana na kuto kujiamini.

Pili unatakiwa utumie nguvu wakati mwingine katika mambo yako bila hivyo huwezi kupata.

Tatu tabia yako ya kupenda kujishughulisha na mambo madogo madogo, kutoa mawazo ambayo hayaendani na hali halisi, na tabia yako ya kutokueleweka na kupenda kusema uongo haikusaidii , achana nayo.


WATU WA NAMBA 3:

Ukiwa umezaliwa tarehe 3, 12, 21 au tarehe 30 au jina lako likianzia na C L na U, tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana kuwa na matamanio makubwa kupita kiasi au kutokuwa na matamanio kabisa.

Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kujionyesha mbele za watu kwamba wewe unajua zaidi kuliko wao.

Tatu tabia yako ya kutaka kudhibiti watu katika mambo yako au katika dili zako inawafanya watu wakukimbie.

WATU WA NAMBA 4:

Ukiwa umezaliwa tarehe 4, 13, 22 au tarehe 31 au jina lako likianzia na D M na V, tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana na wewe kuto jishirikisha na Jamii na kutokuelewa mabo kwa haraka.

Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kushindwa kuonyesha hisia zako

Tatu, achana na tabia yako ya kufanya mambo yasioeleweka hasa kuwa mkali au kununia watu.

WATU WA NAMBA 5:

Ukiwa umezaliwa tarehe 5, 14, au tarehe 23 au jina lako likianzia na E, N na W tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana malengo, dhamira au mwelekeo tangu mwanzo wa maisha yako

Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kuwa na jambo au mtu kwa muda mfupi. Kaa na watu acha kubadili marafiki kila leo

Tatu, tabia yako ya ulevi, ngono, kucheza kamari, kutokuwa muangalifu, ukosefu wa adabu na tabia ya kuchelewesha mambo inachangia wewe kukosa mafanikio.


WATU WA NAMBA 6:

Ukiwa umezaliwa tarehe 6, 15 au tarehe 24 au jina lako likianzia na
F O na X tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana Usumbufu, Ubinafsi na Wivu

Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kusengenya watu na kuingilia mambo ya watu wengine bila hivyo huwezi kufanikiwa.

WATU WA NAMBA 7:

Ukiwa umezaliwa tarehe 7, 16, au tarehe 25 jina lako likianzia na G P na Y tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana kuwa na tabia ya kuwafikiria wenzio mabaya na kutomwamini mtu yoyote

Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kutumia ujanja ujanja katika mambo, uongo au njia za kitapeli kupata fedha.

Tatu tabia yako ya ulevi, Dhihaka, Kupiga vijembe vinakusababisha kukosa mafanikio.

WATU WA NAMBA 8:

Ukiwa umezaliwa tarehe 8, 17, au tarehe 26 au, jina lako likianzia na H Q na Z tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana kutokuelewana na watu na kujifanya kuwa na hisia za huzuni wakati wote, uroho na ulafi, zinakusababisha kukwama.

Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kupenda kujilimbikizia mali, ubahili Uliokithiri na kupenda kuchokoza watu au kuudhi watu vitakukwamisha.

WATU WA NAMBA 9:

Ukiwa umezaliwa tarehe 9, 18, au tarehe 27, jina lako likianzia na I na R tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana na wewe kushindwa kudhibiti maamuzi ya ghafla, hasira za haraka haraka, na unywaji wa pombe

Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kuongozwa na watu wengine na kupenda kubembeleza

Tatu tabia yako ya kupenda ugomvi na ndoto ambazo hazina malengo kunasababisha wewe kukwama kabisa kimaisha

Popular posts from this blog