BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LATAKA WALIOLIPUA ARUSHA

Dar es Salaam.
 Bunge la Afrika Mashariki limeitaka Serikali kuhakikisha linawatia mbaroni watu wote waliohusika na mlipuko wa bomu lililosababisha watu wanne kupoteza maisha na kujeruhi zaidi ya 60.
Katibu wa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Tanzania, Shyrose Bhanji alisema jana kuwa Serikali haina sababu ya kuwafumbia macho, wala kuwaonea haya wahusika kwa kuwa wamegharimu maisha ya watu na kuhatarisha amani.
“Tunalaani mashambulizi ya kinyama yaliyogharimu maisha ya wasio na hatia... tunawataka Watanzania wote kudumisha amani ambayo ndiyo sifa ya Tanzania,” alisema.
Kuhusu Bunge hilo litakalokutana Arusha Agosti na Oktoba mwaka huu, Bhanji alisema tayari miswada miwili imepitishwa; Ukaguzi wa abiria mipakani na ule wa magari ya mizigo barabara za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Bhanji alisema Bunge la Afrika Mashariki limepunguza vituo vya ukaguzi mipakani na kwamba, sasa wote wanaoingia nchi nyingine watakuwa wakikaguliwa kule wanakoingia siyo wanakotoka.
Alisema lengo ni kupunguza urasimu na muda, muda mwingi unapotea kwa ukaguzi.
Popular posts from this blog