Picha-CECAFA YAINGIA NUSU FAINALI

Mashindano ya kandanda ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ya kuwania kombe la Kagame yameingia nusu fainali nchini Sudan sehemu ya Darfur Kaskazini na Kordofan Kusini.
Jumatano wiki hii Express ya Uganda inapimana nguvu na APR ya Rwanda kisha wenyeji Al Ahly Shandy dhidi ya Al Merreikh ya kutoka El Fashir, mji mdogo ambao una uwanja wa kimataifa wa ndege pamoja na viwanja vya kisasa vya voliboli, mpira wa kikapu na kandanda.
Mechi hiyo ya wenyeji inasubiriwa kwa hamu. Al Merreikh ina mashabiki wengi na wachezaji kadhaa wa nje baadhi yao Joseph Kabagambe ambaye ni mchezaji kutoka Uganda wa kiungo cha kati na Adam Williams wa Nigeria. Mchezaji mwingine wa Nigeria David Nwosu anayechezea Merreikh hatacheza kwa sababu ya kuonyeshwa kadi mbili za manjano..
Alhamisi wiki hii Vital'O ya Burundi inapepetana na Ports ya Djibouti mechi ya kwanza ya robo-fainali, na ya pili ni kati ya Rayon ya Rwanda na URA ya Uganda. Mechi za nusu-fainali ni Ijumaa na Jumamosi kisha Julai tarehe mosi ni mechi ya fainali.

Popular posts from this blog