Skip to main content

WATU 37 WAFARIKI DUNIA KWENYE MGODI

Wachimba migodi 37 wameuawa baada ya mvua kubwa kusababisha kuporomoka kwa machimbo walimokuwa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Maafisa wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea Jumapili karibu na mji wa Ndassima, umbali wa kilomita 440 Mashariki mwa mji mkuu,Bangui.
Taarifa zinazohusiana
afrika magharibi
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, siku tatu za kuomboleza zimetangazwa nchini humo.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ina utajiri wa dhahabu na almasi lakini imekumbwa na mzozo wa muda mrefu, baada ya waasi kupindua serikali mwezi Machi.
Msemaji wa rais Prosper Ndouba, alisema kuwa anahofia kuwa watu zaidi huenda wakafariki.
"kufikia sasa idadi ya waliofariki ni 37, ingawa kuna wengi zaidi waliojeruhiwa, '' alisema bwana Ndouba
Afisaa mmoja ambaye hakutajwa jina aliambia shirika la habari la AFP kuwa idadi kubwa ya wachimbaji walikuwa kwenye machimbo hayo yaliyogeuka na kuwa tope baada ya mvua kubwa kunyesha na hivyo kuwaporomokea


Popular posts from this blog

(DjMix) DJ DEO - BONGO FLEVA HITS NON STOP MIXING

Please listen and download this dj mixing from tanzania by group YOUNG DJS ...Present Dj Deo on this mix

(Audio - Dj Mixing) DjDeo - BONGO FLEVA OLD SKOOL NON STOP

This is mix from the Dj in Tanzania who representing YOUNG DJS GROUP ... Make this olds of bongo fleva ....
Take your time to download and to listen of it...If you will like the mix yu can subcribe and comment below or to my whatsapp number.... on the cover ...

KURASA ZA MAGAZETI MBALIMBALI ZATAWALA PICHA ZA MANDELA

Baada ya hapo jana majira ya saa 2 usiku kwa saa za afrika ya mashariki kutangazwa kifo cha aliyekuwa mpigania uhuru na raisi wa kwanza wa Afrika kusini Bw.Nelson Mandela,leo hii magazeti mbalimbali duniani yatawala kwa habari hiyo

ANGALIA MAGAZETI HAYO