Picha - KAJALA AKIWA MAPUMZIKONI MWANZA NA KANISANI

Mwigizaji Kajala Masanja aliyerudi uraiani hivi karibuni baada ya kuachiwa kwa dhamana ya shillingi milioni 5 za kitanzania zilizotolewa na mwanadada Wema Sepetu ameamua kwenda mapumzikoni jijini Mwanza kwa ajili ya mapumziko binafsi ya kutuliza akili yake zaidi akitafakari mipango yake iliyobakia kwa ajili ya mwaka 2013.

Akizungumza na simu tokea na bongo movies tokea jijini humu kajala amesema hii ni safari yake ya kwanza mkoani humo toka atoke jela na atakuwepo kwa siku kadhaa kabla ya kurejea jijini Dar es salaam

Katika moja ya picha mbalimbali alizoweka mtandaoni kajala alionekana kuhuduria kwenye nyumba ya ibada (kanisani) huku akiandika kanisani kidogo kusali muhimu sana nakushukuru mungu kila siku....akiwa pamoja na masista kadhaa wa kanisa hilo la katoliki eneo hilo.

Source Bongomovies.com


Popular posts from this blog