Talk of Today-MASWALI NA MAJIBU

1. Mtu anakupigia simu usiku wa manane halafu anakuuliza "Je umelala?"
Jibu: Hapana, ninachoma mahindi...
2. Uko na demu mahala, unaanza kumchojoa nguo kisha anakuuliza, ni nini unajaribu kufanya..?
Jibu: Nataka kukusaidia kuzifua...
3. Wanakuona unatoka bafuni kuoga ukiwa umeloana, kisha wanakuuliza; "Vipi umetoka kuoga...?"
Jibu: Hapana, nilitumbukia tu kwenye tundu la choo...
4. Unasimama ukingoja lifti ghorofa ya chini ili uende juu ofisini, kisha mtu anakuuliza; "Je unaenda juu..?''
Jibu: Hapana, naisubiri ofisi yangu kuja hapa chini na kunichukua!
5. Mpenzi wako kaja na lundo la maua bado unamuuliza; Je hayo ni Maua...?"
Jibu: Hapana mpenzi, ni magimbi haya..!
6. Upo kwenye boksi la kununulia tiketi kwenye jumba la sinema, kisha jamaa anakuuliza; Unafanya nini hapa..?''
Jibu: Nipo hapa kulipa ada ya Shule..!
7. Wakati watu wanakuona kitandani umelala na macho ukiwa umefunga, bado wanauliza; ''Je umelala....?''
Jibu: Hapana! Najifunza jinsi ya kufa...
8. Unaenda baa kisha muhudumu anakuuliza; "Je naweza kukuletea meza....?''
Jibu: Hapana, ntakunywa hapa kwenye sakafu...!

Popular posts from this blog