"WHY TUNAPUKUTIKA?"-MASTAA WA BONGO WANAJIULIZA

HABARI KUTOKA BONGOMOVIES.

Jana bongo movies tumepata pigo baada ya mwigizaji mwenzetu Jaji Khamis ( kashi) alifariki dunia katika hospitali ya muhumbili alipokuwa amelazwa. Msiba huu unakuwa ni mwendelezo wa majanga na misiba inayowakumba wasanii na watu maafuru nchini ikiwa ni siku chache tuu zimepita toka tulipomzika msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea aliyefariki huko Afrika ya kusini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni utumiaji mkubwa wa dawa za kulevya.
Tukiwa bado kwenye wiki hii ya msiba tumeweza kupata comments za mastaa tofauti wa tasnia ya uigizaji waliyosema jana baada ya taarifa za msiba wa kashi kuwafikia. Ila jambo ambalo limeonekana kuwatatiza wote  jana ni “kwanini maisha ya wasanii yanakatika hivi”? Why?  Ni Swali gumu na ambalo wengi wetu hatuwezi kuwa na jibu moja la uhakika maana Mungu ndo ajuaye yote na muweza yote. Apangalo Maanani hamna anayeweza kulipangua. Cha msingi ni kukaa katika njia zake yeye.
Chini ni baadhi ya maneno waliyosema waigizaji hawa jana.
Wema Sepetu
Innah lillahi wa innah illahi rajoon..... dah tunapukutika tu wallahi.... dah....

Elizabeth Michael (LULU)
Ehhh Mungu wangu!!!mbna tunaisha hv jaman!??? REST IN PEACE DADA CASHY.....uwiii tumrudieni MUNGU jaman...hakuna anayejua siku wala saa.....

Salma Jabu (Nisha)
Ni ngumu kuamini ila huu ndio ukweli ulivyo!!kwanini sisi??hatujamsahau mangwea leo ww dada???whyyyyyyyyy R.I.P dadaaa aaaa CASH WHYYYYYY
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen


Share: