KIWANDA CHA KUTENGENEZA SILAHA TANZANIA CHAGUNDULIKA

Kiwanda cha kienyeji cha kutengeneza vifaa na silaha mbalimbali,kimegundulika kuwepo jijini Dar es Salaam,ambapo wahusika wa kiwanda hicho wamekiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambayo yamesababisha mauaji mengi sehemu mbalimbali. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, kamishna msaidizi wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam DCP Ally Mlege,amesema katika hali ya kushangaza baada ya kukamatwa kwa baadhi ya watuhumiwa waliokuwa wakijihusisha na matukio ya ujambazi,hatimaye baada ya kubanwa na jeshi la polisi walikubali na kusema kiwanda hicho kilichopo maeneo ya Kawe Mzimuni kinatumika katika kutengeneza na kukarabati vifaa na silaha mbalimbali zinazotumika katika matukio ya uporaji na unyang'anyi ambavyo vilitumika na kusabisha mauaji mengi sehemu mbalimbali.
Aidha tapeli hatari bwana Mfaume Omary maarufu kwa jina la Mau(29)mkazi wa Magomeni Kagera,ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kutumia namba tofauti za mitandao ya simu na majina ya watu maarufu ikiwemo viongozi wa serikali na viongozi wa dini kwa lengo la kujipatia fedha kwa kuvaa uhusika wa mtu husika bila wanaombwa fedha hizo kugundua.
Jeshi la polisi limekanusha vikali kuhusu habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuwa mbunge wa jimbo la Ubungo Mh John Mnyika amekoswa na bomu na kumjeruhi moja ya wafuasi wake kuwa ni la huzushi,na ukweli ni kwamba bomu hilo lililipuka ndani ya gari la polisi Pt .1902 wakati askari dcp Julius alipokuwa ndani ya gari akisogeza box lenye mabomu ya machozi na kwa bahati mbaya bomu hilo lililipuka ndani ya gari hilo lakini halikuleta madhara kwa askari polisi yeyote wala raia waliokuwa katika eneo hilo


Share: