MAHAKAMA YA KIMATAIFA ICC YAKATAA OMBI LA RUTO

Kufuatia kesi inayowakabiri Raisi wa Kenya Mh Uhuru Kenyata  na makamu wake William Ruto
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imekataa ombi la makamu rais wa Kenya kutaka kesi yake ianze kusikilizwa Afrika. ICC imesema  kuwa kesi ya makamu rais wa Kenya William Rutto itaanza kusikilizwa mwezi Septemba huko Hague katika makao makuu ya  ICC.

Ruto na mshitakiwa mwenzake Joshua Arap Sang wanashitakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, kwa kusaidia kufanya ghasia mbaya za kikabila zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Mawakili wa utetezi waliiomba ICC kusikiliza walau sehemu ya kesi hiyo nchini Kenya au Tanzania.   Taarifa ya ICC inasema majaji walikubali  kimsingi  wazo hilo lakini wameamua kusikiliza kesi hiyo Hague kwa sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na usalama, gharama na athari kwa mashahidi na waathirika.

Uamuzi huu wa leo hautaathiri kesi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye anakabiliana na mashitaka ya uhalifu  dhidi ya ubinadamu kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi  nchini Kenya.  Kesi yake inatarajiwa kuanza kusikilizwa Novemba 12.


Popular posts from this blog