MAJINA KIDATO CHA TANO YATANGAZWA

Hatimaye leo majina ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha 5 mwaka 2013 yametangazwa na Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo.

Jumla ya wanafunzi 34,482 walikuwa na sifa za kujiunga na kidato cha 5 ila waliochaguliwa ni 33,683, wasichana ni 10,300 na wavulana ni 23,383. Wengine 76 wameachwa kutokana na umri wao kuzidi miaka 25.

Ufaulu katika masomo ya sanaa (Arts) umeshuka sana, na nafasi nyingi za masomo hayo zimebaki wazi bila kupata wanafunzi.

Nafasi za wanafunzi wa masomo ya sayansi 18,564 zote zimejazwa.

Wanafunzi 530, wamechaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya ufundi, kati yao wavulana ni 416 na wasichana ni 114.

Wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha 5, wanatakiwa kuripoti shuleni tarehe 29 mwezi huu wa 7.
Share: