Makala-HAYA MAMBO 20 HUTAKIWI KUFANYA KIJANA

Makosa 20 ambayo hutakiwa kuyafanya kwenye ujana wako:

20. Kufanya kazi kwa ajili tu ya hela wakati kiukweli haikuwa ndoto yako maishani kufanya unachofanya wakati bado una nafasi na uwezo wa kufanya vizuri zaidi kwenye maisha na kuishi ndoto zako.

19. Kufikiria kwamba inakubidi uwe na mpenzi kwa sababu tu umeona wenzako wana wapenzi au wameoa na kuolewa. Usiangalie wenzako na wewe ukaamua kuamua hatma ya maisha yako. Inawezekana unaona wana raha lakini kiukweli wana matatizo makubwa. Oa, penda, olewa kwa sababu unapenda na unaona ni muda muafaka na si kwa sababu fulani na fulani wamefanya.

18. Kujaribu kujifanya umekua badala ya kukua kweli.

17. Kutumia nguvu nyingi kutengeneza marafiki badala ya kutengeneza uaminifu.

16. Kujifanya hujali kwa sababu eti we only live once!

15. Kufanya kila unachotaka kuwa kama mahitaji yako ya msingi. Mfano starehe kupindukia.

14. Kuisahau familia yako, ndugu na jamaa zako.

13. Kurilaksi kama tayari umeshafanikiwa na kila kitu maishani. Unahitaji mapumziko? Angalia umefanya nini cha maana.

12. Kuendelea kufanya kazi miaka na miaka, kazi ambayo haikuongezea kitu chochote kipya kichwani.

11. Kufuata mkumbo badala ya kuwa na misimamo binafsi.

10. Kulaumu watu wengine unapokosea kwenye maisha. Stand up for yourself!

9. Kusahau kutengeneza uhusiano mzuri na watu wanaokuzunguka.

8. Kuacha kujifunza mambo mapya na kujiona umefikia mwisho wa kujifunza.

7. Kufikiria unatenda wema ili ulipwe. Fanya uende zako. No disappointments.

6. Kutumia hela zako na mwanamke au mwanaume ambaye hatakuwa na muda mwingi na wewe kwenye maisha yako. Hamna future.

5. Kung’ang’ania marafiki ambao wanakupotezea muda na hawakuongezei chochote kwenye maisha yako.

4. Kusahau kujiwekea akiba na kutumia bila mpango kila shilingi unayopata.

3. Kusahau kwamba what goes round comes round. Be good to people who deserve it!

2. Kufanya ngono zembe kisha kujilaumu kwa matokeo yake.

1. Kuiga maisha ya watu wengine. Be original.

Source Masanja Mkandamizaji
Share: