MBOWE AJISALIMISHA MAKAO MAKUU YA POLISI DAR

Mhe. Freeman Mbowe, leo majira ya saa 9 na nusu alasiri ameambatana na Mawakili wawili, Nyaronyo Kicheere na Peter Kibatala na kufika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa Mahojiano 
Inadaiwa kuwa anahojiwa juu ya CHADEMA kulihusisha Jeshi la Polisi na Mlipuko Arusha, Tuhuma za CHADEMA kuwa Polisi inatumiwa na CCM katika chaguzi mbali mbali.

Kwa wale ambao mnakumbuka kuwa siku ya ijumaa usiku wa manane Polisi kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakiongozwa na RCO wa Kinondoni walienda nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba usiku kwa lengo la kumkamata, Mbowe alikuwa safarini na alipitia Airport ya Dsm Hivyo kwenda kwake usiku ni jambo la kushangaza sana , leo amerejea kupitia Airport ya Dar na akaamua kwenda moja kwa moja Polisi ili kujua kulikoni.

Aidha mahojiano yao yanahusu mambo yafuatayo;

1.kuwa tamko la kamati kuu kuwa Polisi walihusika na mlipuko wa Bomu Arusha .....itakumbukwa alishahojiwa tena na akina Chagonja na mpaka leo hakuna taarifa zozote wazi.
2. Kuwa Polisi wanatumiwa na CCM ndio maana wanaisaidia Ccm Katika chaguzi mbalimbali ......na hata bomu la Arusha ilikuwa sehemu ya mkakati huo.
3. Kwamba kauli kuwa JK na Bunge kutokuonyesha dalili zozote za kusikitishwa na hata kushindwa kuhudhuria mazishi ni dalili za serikali kuhusika katika tukio hilo.
Popular posts from this blog