Skip to main content

WANAJESHI WALIOKUFA DARFUL-JWTZ KUFANYA UCHUNGUZI

Dar es Salaam. Wakati Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban K-Moon, wamelaani mauaji ya wanajeshi wa Tanzania Jimbo la Darfur, Sudan, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeunda timu ya kuchunguza tukio hilo.
Wapiganaji saba kati ya 36 wa Tanzania waliokuwa kwenye Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa, (Unamid), waliuawa Jumamosi na wengine 19 kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo yalitekelezwa karibu na kambi ya Manawashi eneo la Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alisema Dar es Salaam jana kuwa timu ya wataalamu itakwenda Darfur kuchunguza tukio hilo.
Tukio hilo limekuwa la kushtua, kwani miaka mitano ya majeshi ya kulinda amani kuwa huko haijawahi kutokea mauaji makubwa kiasi kile.
Kanali Mgawe alisema wanawasiliana na UN kufanya taratibu za kurudisha nyumbani miili ya wapiganaji hao.
Taarifa ya Unamid
Taarifa ya iliyotolewa jana na Msemaji wa Unamid, Christopher Cycmanick, ilisema wanajeshi hao waliuawa walipokuwa kwenye doria ya kawaida.
Cycmanick alisema walinzi hao wa amani walishambuliwa kwa bunduki na silaha nzito za kivita umbali wa kilomita 25 kutoka katika kambi yao.
JK atuma salamu za pole
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais Kikwete ameeleza kushtushwa na tukio la kushambuliwa na kuuawa wapiganaji wa JWTZ Mji wa Darfur, Sudan.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu, ilisema Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, familia na wapiganaji wote.
Ban K-Moon
Ki-Moon alisema tukio la kuuawa kwa askari hao haliwezi kuvumilika, ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kubaini wahusika.Ban ameiagiza Serikali ya Sudan kufanya uchunguzi huo katika mazingira ya uwazi na ukweli


Popular posts from this blog

(DjMix) DJ DEO - BONGO FLEVA HITS NON STOP MIXING

Please listen and download this dj mixing from tanzania by group YOUNG DJS ...Present Dj Deo on this mix

(Audio - Dj Mixing) DjDeo - BONGO FLEVA OLD SKOOL NON STOP

This is mix from the Dj in Tanzania who representing YOUNG DJS GROUP ... Make this olds of bongo fleva ....
Take your time to download and to listen of it...If you will like the mix yu can subcribe and comment below or to my whatsapp number.... on the cover ...

KURASA ZA MAGAZETI MBALIMBALI ZATAWALA PICHA ZA MANDELA

Baada ya hapo jana majira ya saa 2 usiku kwa saa za afrika ya mashariki kutangazwa kifo cha aliyekuwa mpigania uhuru na raisi wa kwanza wa Afrika kusini Bw.Nelson Mandela,leo hii magazeti mbalimbali duniani yatawala kwa habari hiyo

ANGALIA MAGAZETI HAYO