HII NDIO MAANA YA "BONGO-BONGO LAND"

Chama cha kibinfasi cha kisiasa cha MEP nchini Uingereza kimeshutumiwa kwa kutumia neno.......'Bongo Bongo Land
Lakini kwa baadhi ya watu nchini Tanzania, neno hilo lina maana isiyo na ubaya wowote.
Mwanachama wa chama hicho, Godfrey Bloom, amenukuliwa kwenye jarida la Guardian akisema,'' inawezekanaje tunatoa msaada wa pauni bilioni moja kila mwezi, kwa 'Bongo Bongo Land' wakati tunakabiliwa na deni kubwa kama hili?''
'Bongo Bongo land' ni neno ambalo hutumiwa miongoni mwa waingereza kama lugha ya dharau kuashiria nchi maskini, au mataifa yanayostawi.
Bloom aliambia BBC kuwa Bongo Bongo Land ni neno wanalotumia watu kuashiria nchi maskini isiyo na ustaarabu.
Hili bila shaka halikumfurahisha Laura Pidcock, mwanaharakati anayepinga ubaguzi wa rangi aliyesema kuwa dhana hizi ambazo watu wanazo kuhusu watu fulani, inarejesha Uingereza nyuma wakati inajipa sifa ya kuwa nchi yenye ustaarabu.
Alisema dhana kama hizo zinapotosha sana.
Wakereketwa wamemtaka kukoma kabisa kutumia tena lugha kama hiyo wakisema kuwa watu katika mataifa ya kigeni watatizama hilo kama ubaguzi wa rangi.
Haya yote yatakuwa habari muhimu kwa watanzania ambako neno hili kwa kifupi,Bongoland lina maana tofauti kabisa na ilivyotafsiriwa na mwanasiasa huyo.
Badala yake inamaanisha mahala ambapo watu wanapaswa kuwa wajanja na kuwa makini wakati wote.
Sehemu hiyo, ni mji mkubwa wa Dar es Salaam. Linatokana na mchanganyiko wa neno la Kiswahili Ubongo - lenye maana Akili,
na neno - land.
Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau anafafanua . "Dar es Salaam ni sehemu ambapo watu hawana budi ila kutumia akili zao. Unaweza kuwa tapeli au mfanyabiashara lakini lazima wawe na mbinu ya kupata pesa.''
Neno hili unaweza kusema ni jipya...kulingana na Famau...limekuwa likitumika kwa miaka 15 sasa. Babake hawezi kuwa analitumia , linatumika sana miongini wa vijana walio chini ya umri wa miaka 35. Lakini linasifika sana kiasi cha kuwahi kuwa jina la filamu iliyotolewa mwaka 2003 kuhusu kijana mmoja mtanzania kuhamia Marekani na fimalu hiyo ikawa na sehemu yake ya pili kwa Bongoland II.
Cha mno zaidi, ikiwa utatumia neno Bongoland nchini Tanzania basi unakuwa umegonga ndipo na kwa hilo unapata pointi hapo wala sio kukosolewa,'' anasema Famau.
Labda ufafanuzi huo ungemsaidia bwana Bloom kujizuia na utata aliosababisha

Godfrey Bloom
Share: