HIKI NDIO KIWANJA CHA KURUKA KILA IJUMAA NA JUMAMOSI

Hii ni club inayomilikiwa na mhindi ambaye aliamua kuwekeza maeneo ya Mbezi beach.Club hii aliyoamua kuipa jina la Ambrosia Bistro n Bar  kutokana na kwamba mmiliki wa eneo hilo ndiyo yule wa zamani aliyekuwa na garden bistro kama unakumbuka.

Hii aliyoijenga ,maeneo ya mbezi beach kwa wale wanaopitia njia ya tegeta wanashuka kituo cha Afrikana kisha unachukua bajaji unamwambia akulete eneo hilo almaaarufu kama BAA YA WAHINDI.
Na wale wanaopitia njia ya kawe wanashuka kituo cha maringo kisha utakuta bajaji zinaenda eneo linaloitwa KWA ZENA unashuka mwisho hapo kwa zena kisha unafuata barabara mbele kidogo utaiona hiyo Ambrosia Bistro

RATIBA YA BURUDANI

Ijumaa na jumamosi na siku zote za sikukuu disko kabambe linapigwa hapo mpaka asubuhi.

KIINGILIO

Siku hizo za disko kiingilio kinakuwa bure kwa wale watakaofika kabla ya saa 4 na kusubiri disko lianze huku wakipata moja moto moja baridi.
Baada ya saa 4 disko likianza kiingilio ni 10000 tu.

WOTE MNAKARIBISHWA.


mAWASILIANO ZIDI 0779 585858





Hali inakuwaga hivi siku za ijumaa na jumamosi
Share: