ALI KIBA ANG'ARA KATIKA TUZO ZA MUZIKI KILL MUSIC AWARDS

Usiku huu kile kinyang'anyiro cha ugawaji wa tuzo za muziki nchini kijulikanaco ka kill muzik awards kimehitimishwa kwa wasanii mbalimbali na makundi mbali mbali ya muziki kupata tuzo hizo.
Lakini kubwa zaidi ambalo limezua gumzo nchini kuwaangalia zaidi wasanii wakubwa wawili wa muziki nchini yaani DIAMOND na ALI KIBA.
Wengi wetu tunajua kuwa kuna ubishani mkubwa sana kati ya wasanii hao wawili mpaka kufikia watanzania wenyew kutengeneza makundi kati yao yaani utakuta kuna TEAM KIBA na TEAM DIAMOND ambapo usiku huu amejidhihilisha mbabe nani katika kuwania tuzo hizo.
Mkoani MTWARA katika baa moja kubwa  inaitwa FIRE CANTEEN hali ilikuwa tete baada ya TEAM hizo mbili kutambiana pindi tu kipenga cha tuzo hizo kilipoanza.
Hali ilianza kutia faraja baada ya DIAMOND kuonyesha matumaini yake mwanzoni katika kipengele cha WIMBO BORA WA MWAKA WA ZOUK RUMBA mbapo wimbo wa NTAMPATA WAPI uliweza kunyakua tuzo hiyo.
Pia katika kipengere kingine cha VIDEO BORA YA MWAKA kupitia wimbo wa MDOGO MDOGO ulimpa tuzo pili DIAMOND.
Hali ikabadilika baada ya ALI KIBA kuanza kushika kasi na kuchukua tuzo 5 katika vipengere hivi....
1.WIMBO BORA WA MWAKA
2.MWIMBAJI BORA WA KIUME(Bongofleva)
3.MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME
4.WIMBO BORA WA AFRO POP na
5MTUNZI BORA WA MWAKA

Kupitia ACCOUNT yake ya INSTAGRAM, Ali kiba Amepost video akiwashukuru wote waliomwezesha kupata tuzo hizo.Kwa sasa ALI KIBA yuko UK katika kazi yake na muziki ndio maana hakuonekana ukumbini wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
Popular posts from this blog