HABARI KUTOKA BONGO MOVIE
Katika hali ya kushangaza na isiyo eleweka mwigizaji Mahsein
Awadhi maarufu kama Dr. Cheni amekumbwa na balaa la kulishwa chakula
chenye sumu weekend iliyopita alipokuwa kwenye sherehe moja ya harusi
jijini Dar es Salaam alipohudhuria kama MC au mshereheshaji wa harusi
hiyo.
Akiongea na bongo movies leo asubuhi, Dr. cheni alisema kuwa
baada ya kumaliza kula chakula ambacho alipakuliwa na mmoja wa wahudumu
wa sherehe hiyo alianza kujisikia vibaya na kuishiwa nguvu na aliamua
kutoka nje kujaribu kupata hewa akidhani ladba ni joto la ukumbini ila
hali ilizidi kuwa mbaya na aliamua kutafuta maziwa akihisi labda inaweza
kuwa vidonda vya tumbo ndipo alipoanza kutapika na baadae kukumbizwa
hospitalini na ndipo alipogungulika kuwa amelishwa chakula chenye sumu.
Tulipomuuliza labda sababu gani anahisi zinaweza kuwa
zimepelekea watu hao kutaka kumdhuru alisema kuwa, mpaka sasa hajaweza
kupata jibu kamili ila anaamini watu waliofanya hivyo wanamfahamu na
wana nia mbaya sana kwake na sio watu wema.
Dr. Cheni alisema kuwa kwa sasa hali yake inaendelea
vizuri na moja ya watu walikuwa wa kwanza kufika hospitalini baada ya
yeye kupatwa na majanga hayo ni mwigizaji Elizabeth Michael (LULU)
ambaye kwa sasa yupo karibu sana na Dr. Cheni aliyekuwa mstari wa mbele
katika kushughulikia mpaka kufanikisha suala la dhamana ya kesi
iliyokuwa inamkabili mwanadada huyo.