Ajali mbaya ya lori lililokuwa limebeba mafuta ya mawese limepinduka jijini dar maeneo ya chang'ombe.Taarifa kutoka kwenye chanzo kimoja cha habari jijini kinasema kuwa lori hilo lilikutana na mkasa huo baada ya dereva wa lori hilo alipotaka kulikwepa gari ndogo aina ya daladala na ndipo lilipopinduka na kugonga magari mengine mawili.
Chakushangaza eneo la ajali hiyo watu walikuwa wakijichotea mafuta huku polisi waliokuwa eneo la tukio kushindwa kufanya lolote.
Dereva wa lori hilo alipatikana na alizungumzia tukio hilo kwa masikitiko makubwa huku akitoa ilani ya wananchi kutokununua mafuta ya mawese.