MTWARA HAKUKALIKI

Ni mapambano baina ya vijana na maaskari.Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA 
 
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . 
 Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
 Mtwara wamefungiwa majumbani tangu asubuhi, huku Jeshi la Polisi likifanya msako wa nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwanasa watuhumiwa wanaodaiwa kuchochea maandamano hayo kwa njia ya vipeperushi
waandamanaji hao wameapa kufa endepo serikali itaendelea na mipango yake ya kusafirisha gesi hiyo hadi Jijini Dar es Salaam.  
Iliyonifikia hivi punde ni kuwa OFISI YA CCM IMECHOMWA MOTO NA MOJA KATI YA VYOMBO VYA HABARI IMEKATA MATANGAZO YAKE KWA MUDA LAKINI HIVI SASA WAMERUDI HEWANI
 
 
 PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO HILO







Share: