GARI LA ZIMAMOTO LAPINDUKA

TAARIFA YA MUDA MFUPI ULIOPITA KUTOKA MTWARA

Gari la zimamoto lililokuwa linawahi kwenda kuzima moto uliokuwa unawaka katika moja ya jengo la ccm lililochomwa moto leo jijini humo kutokana na fujo zilizoanza mapema leo asubuhi lapinduka.Kati ya sababu zilizoelezewa ni kuwa mwendo kasi wa gari hilo ambalo lilikuwa linawahi sehemu ya tukio.
Mpaka sasa yalipotiwa kuwa askari mmoja amejeruhiwa kwa mshale na mmoja wa wananchi amejeruhiwa vibaya na hali yake ni mbaya baada ya kutupiwa kitu kinachodhania kuwa ni bomu.
Share: