Skip to main content

AFYA YA MANDELA BADO UTATA-ZUMA AHAIRISHA ZIARA YAKE YA MSUMBIJI

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefutilia mbali ziara yake ya kwenda Musumbiji baada ya kumtembelea hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema kuwa Bwana Mandela yuko katika hali mbali ya afya.
Msemaji wa Zuma Mac Maharaj amesema kuwa hali yake imedorora zaidi katika saa 48 zilizopita.

Afrika Kusini
Mandela ambaye, ni rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.
Madaktari wanasemekana kufanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Mandela anapona.
Vikundi vya watu wenye huzuni mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela, walikusanyika nje ya hospitali alikolazwa, wakiwa na ujumbe wa ugua pole kwa Mandela
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.
"tutasikitika sana ikiwa tutapata habari za kifo chake, lakini pia tutakuwa tunasherehekea maisha yake. Amefanya mambo mengi zaidi kwa nchi yetu,'' alisema kijana John Ndlovu, mwenye umri wa miaka 25.
Zuma alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa marais nchini Msumbiji, hii leo lakini akaamua kuakhirisha safari yake.
Taarifa kutoka kwa ofisi yake ilisema kuwa anaendelea kuwapongeza wananchi wa Afrika Kusini wanaoendelea kuiombea familia ya Madiba.
Uamuzi wa Rais Zuma kufutilia mbali ziara yake ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa kikanda kuhusu uekezaji anaonyesha wazi kuwa hali ya Mandela inaendelea kuzorota zaidi kulingana na mwandishi wa BBC mjini Johannesburg Mike Wooldridge.Popular posts from this blog

(DjMix) DJ DEO - BONGO FLEVA HITS NON STOP MIXING

Please listen and download this dj mixing from tanzania by group YOUNG DJS ...Present Dj Deo on this mix

(Audio - Dj Mixing) DjDeo - BONGO FLEVA OLD SKOOL NON STOP

This is mix from the Dj in Tanzania who representing YOUNG DJS GROUP ... Make this olds of bongo fleva ....
Take your time to download and to listen of it...If you will like the mix yu can subcribe and comment below or to my whatsapp number.... on the cover ...

KURASA ZA MAGAZETI MBALIMBALI ZATAWALA PICHA ZA MANDELA

Baada ya hapo jana majira ya saa 2 usiku kwa saa za afrika ya mashariki kutangazwa kifo cha aliyekuwa mpigania uhuru na raisi wa kwanza wa Afrika kusini Bw.Nelson Mandela,leo hii magazeti mbalimbali duniani yatawala kwa habari hiyo

ANGALIA MAGAZETI HAYO