Skip to main content

AMBULACE ILIYOMBEBA MANDELA YAHARIBIKA NJIANI KWENDA HOSPITALI

Gari la waGonJwa lililokuwa likimsafirisha hospitalini rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela wiki mbili zilizopita, liliharibika likiwa njiani kwenda hospitalini.

Msemaji wa rais wa Afrika Kusini Mac Maharaj, amethibitisha kuwa gari hilo lilikumba na matatizo na kuwa ilibidi rais huyo wa zamani kuhamishwa hadi gari lingine.
Hata hivyo Bwana Maharaj, amesema tukio hilo halikuwa na tishio lolote kwa afya ya Bwana Mandela, kwa sababu alikuwa na madaktari wa kutosha.
Shirika la habari la Marekani CBS limenukuu vyanzo kadhaa vikidai kuwa Mandela alisalia katika eneo hilo kwa zaidi ya dakika arubaini kabla ya usaidizi kufika.
Shirika hilo la CBS limesema kuwa wakati Bwana Mandela alipokuwa akihamishwa hadi gari lingine viwango vya joto vilikuwa chini sana.
Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alikuwa akisafirishwa kutoka hospitali moja mjini Johannesburg hadi Pretoria, wakati wa tukio hilo lililotokea tarehe nane Juni mwaka huu.
Mandela alilazwa hospitalini huku hali yake ikiwa mbaya kutokana na maambukizi ya mapafu ya mara kwa mara na tangu wakati huo amekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Hii ni mara ya tatu kwa Bwana Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.


Popular posts from this blog

(DjMix) DJ DEO - BONGO FLEVA HITS NON STOP MIXING

Please listen and download this dj mixing from tanzania by group YOUNG DJS ...Present Dj Deo on this mix

(Audio - Dj Mixing) DjDeo - BONGO FLEVA OLD SKOOL NON STOP

This is mix from the Dj in Tanzania who representing YOUNG DJS GROUP ... Make this olds of bongo fleva ....
Take your time to download and to listen of it...If you will like the mix yu can subcribe and comment below or to my whatsapp number.... on the cover ...

KURASA ZA MAGAZETI MBALIMBALI ZATAWALA PICHA ZA MANDELA

Baada ya hapo jana majira ya saa 2 usiku kwa saa za afrika ya mashariki kutangazwa kifo cha aliyekuwa mpigania uhuru na raisi wa kwanza wa Afrika kusini Bw.Nelson Mandela,leo hii magazeti mbalimbali duniani yatawala kwa habari hiyo

ANGALIA MAGAZETI HAYO