USAFIRI WA "MATATU"KUWA NA INTERNET-KENYA

Kama vile Tanzania tuna daladala wenzetu Kenya wanaita matatu ambayo ndio mabasi yao ya jiji.Huko kwa wenzetu wameamua kuweka internet katika mabasi hayo.

Wengi wetu hatupendi zile vurugu za barabarani hususan asubuhi wakati kuna msongamano mkubwa wa magari, inakera na kuudhi. Lakini taswira imebadilika katika uchukuzi wa umma siku hizi mjini Nairobi Kenya, unapokwenda kazini na kurejea nyumbani, unapata mtandao wa internet katika magari ya uchukuzi wa abiria maarufu kama matatu.
Ukiwa ndani ya Matatu hizo unaweza kusoma barua pepe na kusoma habari kwenye mitandao mbali mbali.


Share: