LADY JAY DEE A.K.A ANAKONDA AACHIA NGOMA MPYA "YAHAYA"

Msanii Lady jay dee a.k.a anakonda ambaye ndiyo msanii pekee wa kike anayeshikilia tuzo ya mwanamziki bora wa kike katika tuzo za kill muziki awards,leo hii anatarajiwa kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la YAHAYA.Ngoma hiyoa anatarajiwa kuiachia leo katika kipindi cha power jams cha EAST AFRICA RADIO kinachoruka hewani mchana huu.
Ikiwa zimepita miezi mitatu tangu kuachia ngoma inayofanya vizuri kwa sasa ya JOTO HASIRA akiwa na PROF JAY, mwanadada huyo ameamua kuachia ngoma ya YAHAYA kwani ni moja ya TRACK zinazopatikana katika albamu yake ya NOTHING BUT THE TRUTH ambayo inatarajiwa kutolewa siku ya sherehe yake ya miaka 13 ya muziki kwa "ANAKONDA" siku ya ijumaa pale nyumbani lounge.


Share: